Papa Leo III
Papa Leo III (takriban 750 – 12 Juni 816) alikuwa Papa kuanzia tarehe 26/27 Desemba 795 hadi kifo chake[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2].
Alimfuata Papa Adriano I akafuatwa na Papa Stefano IV.
Leo III amejulikana hasa kwa tendo lake la kumtia Karolo Mkuu taji la Kaisari wa Roma tarehe 25 Desemba mwaka 800.
Leo III alitangazwa na Papa Klementi X kuwa mtakatifu mwaka 1673.
MaishaEdit
Mwenyewe alizaliwa katika familia ya kawaida, akaona upinzani mkali baada ya uchaguzi wake kutoka familia za makabaila wa mji wa Roma waliojaribu kumwua kwa sababu walizoea kuwa na athira juu ya uchaguzi wa Papa wakati ule.
Hivyo Leo alikimbia hadi Ujerumani akitafuta msaada wa Karolo Mkuu mfalme wa Wafaranki. Karolo alimrudisha Roma na walinzi, akafika mwenyewe kuchungulia mashtaka dhidi ya Leo III akaona yalikuwa ya uongo.
Leo III kwa upande wake alijaribu kuimarisha uhusiano wake na Karolo kwa kumvika taji la Kaisari. Hivyo Karolo alikuwa mtu wa kwanza wa kutumia cheo hicho katika mji wa Roma tangu 476, mwaka Kaisari wa mwisho Romulus Augustus alipofukuzwa, na cheo cha Kaisari wa Roma kilipatikana huko Konstantinopoli tu kwa mtawala wa Bizanti.
Tendo la kumwekea Karolo taji hilo lilimkasirisha kiongozi wa Konstantinopoli lakini alikosa nguvu ya kuadhibu Papa au Karolo.
Hivyo Leo III alianzisha ufuatano wa makaisari wa "Dola Takatifu la Kiroma" ulioendelea hadi mwaka 1804.
Tazama piaEdit
Maandishi yakeEdit
- Opera Omnia katika Patrologia Latina ya Migne pamoja na faharasa
TanbihiEdit
Viungo vya njeEdit
- Kuhusu Papa Leo III katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki
- Einhard, Life of Charlemagne (817–830 hivi, tafsiri ya Kiingereza ya mwaka 1880)
- Shughuli au kuhusu Papa Leo III katika maktaba ya WorldCat catalog
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Leo III kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |