Martin Luther King, Jr.
Dr Martin Luther King, Junior (Atlanta, Georgia, 15 Januari 1929 – Memphis, Tennessee, 4 Aprili 1968) alikuwa Mkristo mwenye asili ya Afrika, mchungaji wa Kibaptisti na mwanaharakati mashuhuri kutoka nchi ya Marekani aliyepigania haki za binadamu, hasa Wanegro, wakati nchi hiyo ilipokuwa bado na sheria za ubaguzi wa rangi.
Baadhi ya madhehebu ya Marekani, hasa Waanglikana na Walutheri, yanamheshimu kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe yake ya kuzaliwa au ya kuuawa.
Maisha
haririMartin alizaliwa mjini Atlanta, Georgia, Marekani. Alikuwa mtoto wa mzee Martin Luther King Sr. ambaye pia alikuwa mchungaji na kiongozi wa kupigania haki za binadamu. Baba yake alimwita Martin Luther ili amheshimu huyu mtaalamu Mjerumani wa karne ya 16.
Aliwaongoza Waamerika Weusi kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwepo katika sehemu za USA mpaka miaka ya 1960. Katika mapambano hayo alifuata mapokeo ya Mt. Agostino katika Kanisa. Alieleza ya kuwa kila mtu amepewa na Mungu heshima yake, hivyo sheria za nchi na serikali zinazovunja heshima hiyo si za haki. "Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu" (Mdo. 5:29).
Aliwaita watu kupinga ubaguzi hata dhidi ya serikali na polisi lakini bila kutumia mabavu. Watu waliongozwa na M. L. King waliandamana mahali pengi wakanyamaza wakipigwa na kukamatwa. Wakaingia katika hoteli, shule na vyombo vya usafiri vilivyotengwa kisheria kwa watu weupe, wakasubiri mpaka polisi ilipoitwa na kuwakamata. Wakapokea adhabu na mapigo.
Baada ya miaka kadhaa mapambano kwa silaha hizo za amani yalishinda. Mahakama kuu ya Marekani na serikali kuu zilitangaza ya kuwa ubaguzi wa rangi katika mikoa mbalimbali hauruhusiwi kuendelea.
Mwaka 1964 alipokea Tuzo ya Nobel ya Amani kwa sababu ya kutetea haki bila ya kutumia mabavu.
Hata hivyo aliuawa kwa kupigwa risasi na mteteaji wa ubaguzi wa rangi mwaka 1968.
Baada ya hapo ujumbe wake ulizidi kukubalika na sheria mbalimbali zilibadilishwa.
Anahesabika kama mmoja wa watu wakubwa wa Mungu katika historia ya Kanisa.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Martin Luther King, Jr. - The Atlanta Journal-Constitution. A permanent section of the newspaper dedicated to the life of Dr. King Ilihifadhiwa 16 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.
- The Coalition on Political Assassintions Ilihifadhiwa 5 Mei 2008 kwenye Wayback Machine., A research and lobby group that also organize a conference on the assassination of Dr King.
- This black history resource offers a biography of MLK and links to other related articles. Ilihifadhiwa 17 Februari 2009 kwenye Wayback Machine.
- Photo Essay: The Last Days of Martin Luther King Jr. Dr. King's life and death recalled in images on Time.com (a division of Time Magazine)
- The Martin Luther King, Jr. Papers Project Ilihifadhiwa 30 Oktoba 2010 kwenye Wayback Machine.
- The King Center
- National Civil Rights Museum
- MLK Online Martin Luther King Jr. Speeches, Pictures, Quotes, Biography, Videos, Information on MLK Day and more!
- Martin Luther King Jr.'s, A New Sense of Direction (1968) article Ilihifadhiwa 25 Aprili 2010 kwenye Wayback Machine. published in WorldView magazine.
- Martin Luther King Jr.'s FBI file
- Department of Justice investigation on King assassination
- Martin Luther King in New York Ilihifadhiwa 24 Aprili 2008 kwenye Wayback Machine.
- Martin Luther King Jr. Photographs Ilihifadhiwa 2 Aprili 2007 kwenye Wayback Machine. Photos by Benedict J. Fernandez
- The Seattle Times: Martin Luther King Jr.
- Winner of the 1964 Nobel Prize in Peace
- About.com's Lesser Known Wise and Prophetic Words of Rev. Martin Luther King, Jr. Ilihifadhiwa 10 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Speeches of Martin Luther King
- Pamphlet on King and Socialism from the Socialist Party USA (PDF)
- "The MLK you don't see on TV" from FAIR
- The Martin Luther King Center (German)
- Works by Martin Luther King, Jr. katika Project Gutenberg
- 1956 Comic Book: "Martin Luther King and the Montgomery Story"
- Kirk, John A. New Georgia Encyclopedia Short Biography Ilihifadhiwa 24 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Declassified document, FBI's letter urging him to commit suicide.
- Dyson, Michael Eric. No Small Dreams: The Radical Evolution of MLK's Last Years. LiP Magazine, Januari 2003
- Wise, Tim. Misreading the Dream: The Truth About Martin Luther King Jr. and Affirmative Action. LiP Magazine, Januari 2003
- Summary of plagiarism controversy
- Shelby County Register of Deeds documents on the Assassination Investigation Ilihifadhiwa 4 Januari 2009 kwenye Wayback Machine.
- Shughuli au kuhusu Martin Luther King, Jr. katika maktaba ya WorldCat catalog
- Transcript of interview with Dr. Kenneth Clark
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |