Wanda Alston

Mwanaharakati na Afisa wa serikali

Wanda Alston (Aprili 7, 1959 - Machi 16, 2005) alikuwa mtetezi wa haki za wanawake, mwanaharakati, na afisa wa serikali wa nchini Marekani.

Mnamo miaka ya 1990, Alston alihudumu katika Shirika la National Organization for Women (NOW) kama mtendaji msaidizi. Pia alikuwa kiongozi mwaka 1995 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake wa Beijing. Alikuwa mratibu wa kisiasa katika maandamano matano huko Washington na San Francisco. Alikuwa mjumbe aliyechaguliwa na Bodi ya Taifa ya Wakurugenzi wa shirika la NOW.

Alston pia alifanya kazi kama mshauri wa kisiasa na alikuwa hai katika Chama cha Democratic Party. Pia alifanya kazi kama mratibu wa matukio katika kampeni ya Haki za Kibinadamu. Pia alikuwa katika harakati za uokoaji huko Washington. Vile vile Alston alikuwa mshiriki hai katika kanisa lake la mtaa, Unity Churchy la Washington.[1]

Alston pia alikuwa kiongozi katika jumuiya ya mashoga na alikuwa kaimu mkurugenzi wa Washington, D.C. katika Ofisi ya Wasagaji, Mashoga, Wenye jinsia mbili na Waliobadili jinsia kutoka mwaka 2004 hadi kifo chake.

Alston alifariki mnamo Machi 16, 2005, kama matokeo ya mauaji katika nyumba yake huko Washington, D.C. Alichomwa kisu hadi kufa.[2]

Marejeo hariri

  1. "Women In The Life Association". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-01. Iliwekwa mnamo 2022-02-24. 
  2. Arrest Made in Alston Slaying (washingtonpost.com)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanda Alston kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.