Uzoroasta

(Elekezwa kutoka Waparsi)

Uzoroasta ni dini na falsafa inayopata jina lake kutoka nabii wake Zoroasta au Zarathustra, ambayo iliathiri imani ya Uyahudi na ya dini zilizotokana na Uyahudi.

Wazoroasta wanaamini katika ulimwengu na Mungu apitaye fikira, Ahura Mazda, ambaye ibada zote zinaelekezwa kwake.

Kiumbe cha Ahura Mazda ni asha, ukweli na mpango, ambaye anazozana na kinyume chake, druj, uongo na machafuko.

Kwa sababu binadamu ana hiari, watu lazima wawe na uwajibikaji kwa maadili wanayoyachagua. Kwa kutumia hiari, watu lazima wawe na jukumu tendaji katika mgogoro wa dunia nzima, na mawazo mema, maneno mema na matendo mema ili kuhakikisha furaha na kuepuka machafuko.

Zamani dini iliyo ilikuwa kubwa, lakini siku hizi imebaki na wafuasi 127,000 hadi 190,000 tu. Jumuiya ya takriban Wazoroasta 25,000 [1]wanaishi katika nchi ya asili yao Uajemi (Iran), hasa katika mazingira ya Kerman na Yazd, na pia katika miji mikubwa kama Tehran. Jumuiya kubwa nyingine yenye watu 57,264 inapatikana Uhindi wanapojulikana kwa jina la Waparsi ("Parsee"); wametokana na Wazoroasta kutoka Uajemi waliokimbilia Uhindi wakati jumuiya yao ilipoteswa katika nchi ya asili.

Kutoka Uajemi na Uhindi walihamia mara nyingi kwa hiyo leo hii kuna jamii zao pia Marekani, Kanada na Ulaya. Idadi yao inapungua polepole kwa sababu ni wagumu sana kupokea waumini wapya kutoka dini nyingine ilhali hawakubali tena watoto wao kuwa Wazoroasta wakifunga ndoa nje ya jumuiya.

Marejeo

hariri
  1. Iran is young, urbanized and educated, makala katika gazeti The National kuhusu matokeo ya sensa ya Iran mwaka 2012, iliangaliwa Oktoba 2018
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.