Watemi

(Elekezwa kutoka Wasonjo)

Watemi (au Wasonjo) ni watu wa kabila kutoka eneo la Arusha, nchini Tanzania, karibu na mpaka wa Kenya.

Mwaka 2002 idadi yao ilikadiriwa kuwa 30,000 [1].

Lugha yao ni Kitemi.

Ni miongoni mwa makabila machache nchini yenye idadi ndogo ya watu kwa sababu ya mauaji waliyowahi na wanayoendelea kufanyiwa na koo za Kimasai. Hii ilipelekea kutawanyika na kutengeneza makabila mengine ya Kibantu kama Waikoma.

Asili yao ni Ethiopia, kwenye Blue Nile hadi sehemu za Kenya (Ngurumani) walipopambana na Waluhya hadi sehemu za Engaruka na sasa bonde la Batemi.

Kabila hili linakaribiana na tamaduni za Wamasai, ila tofauti yao ni kwamba Wasonjo wanalima sana na pia wanajenga nyumba za kudumu za kisasa. Kwa kuwa wanaheshimu na kuthamini mila na desturi zao, mbali na mamlaka ya serikali, wanaongozwa kwa kiasi kikubwa na wakuu wa mila (Wenamiji). Hao wana jukumu la kulinda na kuelekeza mila na desturi; hii ni pamoja na kulinda vyanzo vya maji. Pia wana mamlaka ya kutoa hukumu ya haki kwa wakosaji.

Pamoja na mengine, Wasonjo pia hudumisha mila ya ukeketaji kwa wasichana, binti wengi wakifanyiwa ukeketaji wakiwa bado watoto wadogo au katika umri wa kati.

Wasonjo wanawake ni waaminifu sana wanapoolewa, hii inatokana na tamaduni zao jinsi walivyokuzwa. Ila wanaume wao wana wivu sana kwa wanawake wao hasa wakiona mtu wa kabila lingine anaWAendea.

Silaha kubwa ya Wasonjo ni mishale ya sumu ambayo huitumia hata kuwapiga wanaume wakwale.[2] Kwa hiyo Wasonjo, ingawa ni kabila dogo sana, linaogopwa sana na Wamasai ukanda wa Loliondo.

Watemi wanatumia vyakula vya asili kwa sehemu kubwa.

Kazi zao za asili ni kilimo cha umwagiliaji na cha mvua na sasa ni pia wafugaji wazuri. Wanazalisha mahindi na maharagwe, pia mtama na alizeti, mbogamboga zikiwemo nyanya bila kusahau ndizi ambazo zinapendwa na kutumiwa sana wilayani.

Watemi pia ni wafanyabiashara wajasiriamali ambao wameteka eneo lote la wilaya ya Ngorongoro kwa kufanya biashara.

Watemi wameiga uzalendo wa Wachagga wa kujenga nyumba nzuri za kisasa katika vijiji vyao na wameanza kuondokana na nyumba zao za asili za tembe zinazoezekwa kwa nyasi.

Upande wa elimu Watemi wametawanyika Tanzania na duniani wakiitafuta maana miaka ya 1960 ni asilimia ndogo sana waliopata furusa ya kusoma, miaka ya nyuma hawakuweza kupata nafasi hiyo kwa sababu ya Wamasai kuwaonea na kuwafanyia mauaji, ila kwa sasa kabila hilo wamesoma sehemu mbalimbali.

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Watemi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.