Wikipedia ya Kiafrikaans
Wikipedia ya Kiafrikaans (kwa Kiafrikaans: Afrikaanse Wikipedia) ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kiafrikaans. Mradi huu ulianzishwa tarehe 16 Novemba 2001, na ilikuwa Wikipedia ya 11 kuanzishwa.[1]
Kisara | http://af.wikipedia.org/ |
---|---|
Ya kibiashara? | Hapana |
Aina ya tovuti | Mradi wa Kamusi Elezo ya Internet |
Kujisajiri | Hiari |
Lugha asilia | Kiafrikaans |
Mmiliki | Wikimedia Foundation |
Tarehe 13 Mei 2009, toleo hili lilipita makala 12,000[2] na mwaka 2021 limezidi makala ya 100,000, likiwa toleo la 71 kwa ukubwa.
Awali lilikuwa toleo kubwa la Wikipedia katika lugha za Kiafrika, na pia lilikuwa toleo la kwanza la Wikipedia ya lugha za Kiafrika kupita makala zaidi 10,000[3]. Kwa sasa toleo la Kiarabu cha Misri linaongoza kwa mbali sana. Baada ya Kiafrikaans, zinafuata Wikipedia ya Kimalagasi na Wikipedia ya Kiswahili.
Mbali na Waafrika Kusini, Wikipedia pia uhaririwa na watu wa kule Uholanzi, Ubelgiji, Namibia, Ujerumani na baadhi yao kutoka nchi za Skandinavia.[4]
Marejeo
hariri- ↑ "Wikipedia:2001", English-language Wikipedia (16 Desemba 2006)
- ↑ Afrikaans Wikipedia statistics page
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-14. Iliwekwa mnamo 2009-08-04.
- ↑ Meta-Wiki's list of language Wikipedias ordered by size
Viungo vya nje
hariri- Statistics for Afrikaans Wikipedia by Erik Zachte
- Afrikaans Wikipedia a tiny giant Ilihifadhiwa 6 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.