(makala hii inahusu wilaya ya Ubungo, kuangalia makala ya kata ya Ubungo bonyeza hapa)


Wilaya ya Ubungo
Wilaya ya Ubungo is located in Tanzania
Wilaya ya Ubungo
Wilaya ya Ubungo

Mahali pa Ubungo katika Tanzania

Majiranukta: 6°47′42″S 39°15′58″E / 6.79500°S 39.26611°E / -6.79500; 39.26611
Nchi za Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Ubungo

Wilaya ya Ubungo ni jina la mojawapo kati ya wilaya 5 za Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 16000.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 1,086,912 [1].

Ubungo ilifahamika sana nchini kama kitovu kikuu cha Mabasi yaelekeayo mikoani na miji mbalimbali ya Tanzania kama vile Arusha, Moshi, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Iringa, Mtwara, Lindi, Singida, Tanga na Mwanza; vilevile hadi Nairobi, Lilongwe, Lusaka na miji mingine kadhaa ya Afrika ya Mashariki.

Pia Ubungo ina barabara za juu na makao makuu ya Tanesco, shirika la umeme la Tanzania.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Ubungo - Mkoa wa Dar es Salaam - Tanzania  

Goba | Kibamba | Kimara | Kwembe | Mabibo | Makuburi | Makurumla | Manzese | Mbezi | Mburahati | Msigani | Saranga | Sinza | Ubungo