Yohane Calabria (Verona, 8 Oktoba 1873 – Verona, 4 Desemba 1954) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki kutoka Veneto, Italia Kaskazini.

Picha yake halisi.

Alianzisha mashirika ya kitawa ya Watumishi Fukara wa Maongozi ya Mungu kwa wanaume na kwa wanawake[1] yamsaidie kukabili matatizo ya jamii hasa upande wa vijana[2].

Yote hayo yalitokana na huruma yake kubwa kwa maskini, ili kuwatimizia mahitaji yao duniani kote.

Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kwanza mwenye heri tarehe 17 Aprili 1988, halafu mtakatifu tarehe 18 Aprili 1999[3] .

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Ann. Pont. 2007, p. 1490.
  2. Saint Giovanni Calabria. Saints SQPN (3 December 2015). Iliwekwa mnamo 23 September 2016.
  3. "St. Giovanni Calabria", Vatican News Service
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.