Roko, Alfonso na Yohane

(Elekezwa kutoka Yohane wa Castillo)

Roko, Alfonso na Yohane (walifariki Caaró, leo nchini Brazil, 15 Novemba na 17 Novemba 1628) walikuwa mapadri wa shirika la Yesu ambao walifanya umisionari kati ya Waindio, wenye kuishi kwa ufukara mkubwa, wakianzisha kwa ajili yao vijiji vilivyoitwa reducciones, ambapo kazi na maisha ya kijamii viliungana vizuri na tunu za Ukristo, na kwa sababu hiyo waliuawa na mtu aliyetumwa na mganga wa kienyeji.[1].

Wafiadini wote watatu. Mt. Yohane wa Castillo uko upande wa kulia.
Mt. Roko Gonzalez.
Sanamu ya Mt. Alfonso Rodriguez-Olmedo.

Alfonso (alizaliwa 1599 [2]) na Yohane (alizaliwa 1595 [3]) walitokea Hispania, kumbe Roko alizaliwa Asuncion, katika Paraguay ya leo (mwaka 1576).

Wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu wafiadini. Kwanza walitangazwa wenye heri na Papa Pius XI tarehe 28 Januari 1934, halafu watakatifu na Papa Yohane Paulo II tarehe 16 Mei 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 15 Novemba, ingawa Yohane alifariki siku mbili baadaye [4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Clement J. McNaspy, S.J.: Conquistador without Sword. The Life of Roque González, S.J., Chicago, Loyola University Press, 1984, 206pp.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.