Open main menu
Mt. Yohane wa Dukla.

Yohane wa Dukla (kwa Kipolandi Jan z Dukly) alikuwa mtawa na padri wa shirika la Ndugu Wadogo kutoka Polandi[1]

MaishaEdit

Yohane alizaliwa Dukla, Polandi, mwaka 1414 akafariki mwaka 1484 huko Lviv, leo nchini Ukraina.[2]

Ingawa alijiunga kwanza na Ndugu Wadogo Wakonventuali, baadaye akajiunga na urekebisho wa Observansya.

Hata baada ya kupofuka aliendelea kuandaa hotuba zake maarufu kwa kurudisha watu wengi kwenye Kanisa.[2]

Heshima baada ya kifoEdit

Mara baada ya kifo chake aliheshimiwa kama mtakatifu na miujiza mbalimbali ilisemekana kutokea kaburini pake.

Hatimaye, tarehe 10 Juni 1997, Papa Yohane Paulo II alimtangaza rasmi kuwa mtakatifu katika misa aliyoadhimisha huko Krosno, Poland, wakishiriki watu milioni 1 hivi. Sikukuu yake ni tarehe 28 Septemba.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

  • Jones, Kathleen (2006). Butler's Lives of the Saints. New York: Continuum International Publishing Group. ISBN 0-86012-255-7. 

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yohane wa Dukla kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.