Yohane wa Montemarano

Yohane wa Montemarano (Montemarano, Avellino, karne ya 11 - Montemarano, 14 Aprile 1095) alikuwa askofu wa kwanza wa Montemarano, Italia Kusini, kuanzia mwaka 1084 anayesifiwa kwa ukarimu wake kwa maskini na kwa juhudi za kurekebisha maadili ya wakleri wa jimbo lake[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Pius X mwaka 1906.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Aprili[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.