Yosefu Allamano
Yosefu Allamano (Castelnuovo Don Bosco, Asti, 21 Januari 1851 – Torino, 16 Februari 1926) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Italia.
Baada ya baba yake kufariki mapema, alilelewa Kikristo sana na mama yake, dada wa mtakatifu padri Yosefu Cafasso, halafu na mtakatifu padri Yohane Bosco.
Kisha kupata upadrisho, akihudumia patakatifu pa Bikira Maria "Konsolata" (yaani "Mfarijiwa") alianzisha mashirika mawili ya kitawa yenye karama ya umisionari: Wamisionari wa Consolata (I.M.C.) kwa wanaume, na Masista Wamisionari wa Consolata kwa wanawake.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 7 Oktoba 1990.