Yosefu Cafasso (kwa Kiitalia Giuseppe Cafasso; 15 Januari 1811 - 23 Juni 1860) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mwanaharakati kutoka Piemonte, Italia.

Mt. Yosefu Cafasso.

Pamoja na watakatifu Yosefu Benedikto Cottolengo, Yohane Bosco, Maria Dominika Mazzarello na Leonardo Murialdo aliwajibika kukabili matatizo ya jamii katika mji mkuu wa ufalme wa Sardinia, Torino. Hasa alishughulikia wafungwa na waliohukumiwa kufa ili kuwapatanisha na Mungu.

Pia aliwajibika kwa malezi ya kielimu na ya kiroho ya wenye wito wa upadri[1]

Cafasso alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri mwaka 1925, halafu na Papa Pius XII kuwa mtakatifu mwaka 1947.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo ya Kiswahili

hariri
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 216-217
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 181-182

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.