Zubani Shimali
Zubani Shimali (kwa Kilatini na Kiingereza: Zubeneschamali; pia α Beta Librae, kifupi Beta Lib, α Lib) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Mizani (Libra).
(Beta Librae, Zubeneschamali) | |
---|---|
Kundinyota | Mizani (Libra) |
Mwangaza unaonekana | 2.61 |
Kundi la spektra | B8 V |
Paralaksi (mas) | 17.62 |
Umbali (miakanuru) | 185 |
Mwangaza halisi | -1.16 |
Masi M☉ | 3.5 |
Nusukipenyo R☉ | 4.9 |
Mng’aro L☉ | 130 |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | 12300 |
Majina mbadala | Lanx Borealis, β Lib, 27 Librae, BD-08° 3935, FK5 564, HD 135742, HIP 74785, HR 5685, NSV 7009, SAO 140430 |
Jina
haririZubani Shimali ilijulikana na mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hilo kutoka kwa Waarabu wanaotumia neno الزبان الشمالي al-zuban ash-shamali kwa maana ya « koleo la Kaskazini » yaani koleo la nge. Maana yake nyota hii pamoja nyingine za Mizani zilihesabiwa zamani kuwa sehemu ya Akarabu (Nge) na kutazamiwa kama makoleo yake. Hivyo kundinyota lote la Mizani bado liliitwa “Χηλαι” (helai - makoleo) na Klaudio Ptolemaio katika Almagesti. Kwa nyota aliita “ile angavu kwenye ncha ya koleo la kaskazini”[2].
Kwa matumizi ya kimataifa UKIA ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota ya Lib β kwa tahajia ya "Zubeneschamali" [3].
Beta Librae ni jina la Bayer; Beta ni herufi ya pili katika Betabeti ya Kigiriki lakini Zubani Shimali ni nyota angavu zaidi na hii ni mfano ya kwamba Bayer hakufuata mwangaza kamili wakati wa kuorodhesha nyota.
Tabia
haririα Beta Librae iko kwa umbali wa miakanuru 185 kutoka Jua letu. Vipimo vya spektra vinaonyesha ya kwamba iko mwanzoni kwenye safu kuu ya nyota ikipangwa katika kundi la spektra B8. Maana yake ina jotoridi kubwa, inang‘aa sana na kubiringia haraka kwenye mhimili wa mzunguko wake.
Iko katika mchakato wa kuyeyunganisha hidrojeni yake kuwa heli. Kwa kawaida nyota za aina hii zinaonekana nyeupe au buluu kutokana na jotoridi kubwa usoni lakini Zubani Shimali inaonekana kwa rangi ya kijani kwa watazamaji wengi. Ni nyota ya pekee inayoonekana hivyo kwa watu wengine lakini si watazamaji wote wanaokubali.
Tanbihi
hariri- ↑ ling. Knappert 1993
- ↑ Kigiriki: τῶν ἐπ´ ἂκρας τῆς νοτίου χηλῆς ὁ λαμπρός toon ep akras tes notiou heles ho lampros, Heiberg (1903) uk. 106
- ↑ Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
Marejeo
hariri- Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 437 (online kwenye archive.org)
- Caballero, J. A. (May 2010), "Reaching the boundary between stellar kinematic groups and very wide binaries. II. α Librae + KU Librae: a common proper motion system in Castor separated by 1.0 pc", Astronomy and Astrophysics, 514: A98 online hapa
- Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
- J.L. Heiberg: Claudii Ptolemaei opera quae extant omnia Vol. I, Syntaxis Mathematica, Pars II libros VII-XIII continens; Leipzig, Teubner 1903 (Maandiko yote yaliyopo ya Klaudio Ptolemaio)
Viungo vya Nje
hariri- Constellation Guide:Libra
- Libra, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, Star Tales, iliangaliwa Oktoba 2017
- Zubeneschamali (Beta Librae), kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zubani Shimali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |