Ahmedabad ni jiji kubwa katika jimbo la Gujarat kwenye magharibi ya Uhindi, pia ni makao makuu ya mkoa wa Ahmedabad. Ilikuwa mji mkuu wa Gujarat tangu mwaka 1960 hadi 1970.[1] Jiji liko kwenye ufuko wa mto Sabarmati[2]n a kupakana na mji mkuu mpya Gandhinagar.

Ahmedabad
Nchi Uhindi
Jimbo / Mkoa Gujarat
Anwani ya kijiografia 23.03,72.58
Kimo mita 53
Eneo 8,087 km2
Wakazi 7,486,573 (2,014)
Msongamano wa watu 12,000/km2
Simu 079

Eneo la jiji ni kama km28,087 na mkoa wote una wakazi 7,486,573 (2014), ilhali mji wenyewe una wakazi 6,357,693.[3]

Historia hariri

Ahmedabad ilianzishwa na sultani Ahmed Shah mnamo mwaka 1411 BK[4] upande wa mashariki wa mto Sabarmati.

Mwaka 1487 mji ulizungushiwa ukuta wenye urefu wa km 10. Ukuta huu ulikuwa na mageti 12.[5]

Mnamo mwaka 1573 Ahmedabad ilivamiwa na milki ya Mughali na kuwa sehemu yake.[6]

Mwaka 1758 ilihamishwa kutoka Wamughali kwenda utawala wa Wamaratha. Chini ya utawala wao ilikuwa na tasnia ya vitambaa vilivyouzwa hadi Ulaya.

Mnamo mwaka 1818 mji ulifikishwa chini ya utawala wa Kampuni ya Kiingereza kwa Uhindi ya Mashariki. Tangu mnamo 1850 viwanda vya nguo vilianzishwa Ahmedabad na mji ulikuwa kitovu cha tasnia hiyo nchini. Hivyo ilitwa mara nyingi "Manchester of the East" kwa kulinganishwa na mji ule wa Uingereza wenye viwanda vingi vya nguo.

Katika karne ya 20 mji ulikuwa muhimu katika harakati ya kupigania uhuru wa Uhindi. Mahatma Ghandi aliunda vituo viwili vya harakati hiyo karibu na mji, na mwaka 1930 alianzisha hapa maandamano ya chumvi iliyokuwa hatua muhimu kukabili mamlaka ya ukoloni wa Kiingereza.

Wakati wa uhuru na ugawaji wa Uhindi Ahmedabad iliona mapigano makali baina ya Wahindu na Waislamu na wakimbizi wengi Wahindu kutoka Pakistan walihamia hapa.

Uchumi hariri

Ahmedabad imeendelea kuwa mji wa viwanda[7]. Pamoja na viwanda vya nguo[8] kuna pia viwanda vya magari ya kampuni za Tata na Peugeot [9] na madawa.[10]

Usafiri hariri

Reli hariri

Ahmedabad ni sehemu ya mtandao wa reli ya Uhindi. Kituo cha Kalupur iko katikati ya jiji kinaunganishwa na mfumo wa metro na mabasi ya mwendokasi.[11]

Barabara hariri

Mji unaunganishwa na mfumo wa barabara kuu za kijimbo na kitaifa.

Usafiri kwa ndege hariri

Ahmedabad inahudumiwa na Uwanja wa Ndege wa Sardar Vallabbhai Patel[12] ulioko kwa umbali wa kilomita 9 kutoka kitovu cha jiji ukihudumia pia mji mkuu wa Gandhinagar.

Marejeo hariri

  1. Incredible India | Gujarat. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-08-24. Iliwekwa mnamo 2019-09-05.
  2. Kumar, Rita. N.; Solanki, Rajal; J.I, Nirmal Kumar (2011). "AN ASSESSMENT OF SEASONAL VARIATION AND WATER QUALITY INDEX OF SABARMATI RIVER AND KHARICUT CANAL AT AHMEDABAD, GUJARAT.". EJEAFChe 10 (5). ISSN 1579-4377.  Unknown parameter |eissn= ignored (help)
  3. About Ahmedabad | About Us | Collectorate - District Ahmedabad. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-08-24. Iliwekwa mnamo 2019-09-05.
  4. Samaddar, Ranabir (2016-05-26). Neo-Liberal Strategies of Governing India (in English). Routledge. p. 279. ISBN 9781317199694. 
  5. Kuppuram, G. (1988). India through the ages: history, art, culture, and religion (in English). Sundeep Prakashan. 
  6. See Stunning Architecture in India's First World Heritage City (2018-04-25).
  7. Spodek, Howard (1969). "Traditional Culture and Entrepreneurship: A Case Study of Ahmedabad". Economic and Political Weekly 4 (8): M27–M31. ISSN 0012-9976. JSTOR 40737346. 
  8. Perry, Victoria (2015). Forty Ways To Think About Architecture (in English). John Wiley & Sons, Ltd. pp. 249–253. ISBN 9781118822531. doi:10.1002/9781118822531.ch38. 
  9. Jan 31, Piyush Mishra | TNN | Updated:. Rise of an Auto hub | Ahmedabad News - Times of India (en).
  10. Dutta, Vishal. "Gujarat's contribution surged in pharma, to become global hub: ASSOCHAM", The Economic Times, 2013-04-30. 
  11. Aug 27, Himanshu Kaushik | TNN | Updated:. World Heritage Site: Next stop for heritage makeover is Kalupur railway station | Ahmedabad News - Times of India (en).
  12. Sardar Vallabbhai Patel International Airport, AAI. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-12-14. Iliwekwa mnamo 2019-09-05.

Viungo vya Nje hariri

 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: