Aleksanda I wa Aleksandria

(Elekezwa kutoka Aleksanda wa Aleksandria)

Aleksanda I wa Aleksandria (alifariki tarehe 26 Februari[1] au 17 Aprili, 326 au 328) alikuwa Patriarki wa 19 wa Aleksandria, Misri. Wakati wa uongozi wake alikabili masuala mbalimbali, kama vile tarehe ya Pasaka, matendo ya Meletius wa Lycopolis, na hasa Uario. Ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa padri Ario na wa mafundisho yake hadi Mtaguso wa kwanza wa Nisea. Ndiye aliyemuandaa shemasi Atanasi wa Aleksandria kuwa mwandamizi wake.[2]

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu[3].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Februari[4] au 29 Mei[5].

MaandishiEdit

Mengi kati ya maandishi yake hayakutufikia, isipokuwa barua mbili. Mengine hayana hakika.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

  • Alexander I (313–328). Official web site of the Greek Orthodox Patriarchate of Alexandria and All Africa. Iliwekwa mnamo 2011-02-08.

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.