Almurabitun (kutoka Kiarabu: المرابطون‎, kwa Kiingereza: Almoravids) walikuwa nasaba ya Waberberi [1] kutoka Sahara iliyotawala eneo pana la kaskazini magharibi mwa Afrika na Rasi ya Iberia wakati wa karne ya 11.

Bendera ya Almurabitun

Chini ya nasaba hiyo milki yao ilitawala Moroko ya leo, Sahara ya Magharibi, Mauritania, Gibraltar, Tlemcen (leo nchini Algeria) na sehemu kubwa ya nchi ambazo sasa ni Senegal na Mali, pamoja na Hispania na Ureno upande wa Ulaya. Wakati wa kilele chake, milki ilikuwa na upana wa kilomita 3,000 kutoka kaskazini hadi kusini.

Watawala wao walitumia Aghmat (1040-1062) na Marrakech(1062-1147) pamoja na Córdoba kama miji mikuu.

Uvamizi wa Almurabitun upande wa kusini mwa jangwa la Sahara ulikuwa muhimu kwa uenezaji wa Uislamu ukisababisha watawala kadhaa wa Kiafrika kuwa Waislamu, kwa mfano wafalme wa Mali na Dola la Songhai.

Watawala hariri

  • Abdallah ibn Yasin (1040-1059)
  • Yusuf ibn Tashfin (1061-1106)
  • Ali ibn Yusuf (1106-42)
  • Tashfin ibn Ali (1142-46)
  • Ibrahim ibn Tashfin (1146)
  • Ishaq ibn Ali (1146–1147)

Tanbihi hariri

  1. Glick, Thomas F. Islamic And Christian Spain in the Early Middle Ages. (2005) Brill Academic Publishers page 37

Marejeo hariri

  • Historia Kuu ya Afrika, Afrika kutoka Saba hadi Karne ya kumi na moja, Mh. M. Elfasi, Ch. 13 I. Hrbek na J. Devisse, The Almoravids (uk. (336-366), UNESCO, 1988
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Almurabitun kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.