Andrea Bessette (maarufu kama Frère André; Mont-Saint-Grégoire, 9 Agosti 1845Montréal, 6 Januari 1937), alikuwa bradha wa shirika la Msalaba Mtakatifu nchini Kanada.

Picha yake halisi.

Alizaliwa katika familia ya kawaida yenye watoto wengi, akawahi kubaki yatima na kukabidhiwa kwa utunzaji wa shangazi. Alifanya kazi katika kiwanda cha nguo huko Kanada na Marekani .

Mwaka 1870 aliingia utawani akapewa kazi ya bawabu wa ofisi ya chuo cha Notre-Dame huko Montreal.

Alikuwa na sifa kama mponyaji [1].

Alithibitishwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri mnamo 1982, Papa Benedikto XVI akamtangaza mtakatifu tarehe 17 Oktoba 2010.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.