Andy Chande
Jayantilal Keshavji (pia hujulikana kama Andy Chande; 7 Mei 1928 – 7 Aprili 2017) alikuwa mfanyabiashara mkubwa, mhisani na mwanachama wa chama cha Freemasons aliyeheshimika kama mtu aliyefanya mambo yenye kuleta matokeo makubwa katika nchi yake ya Tanzania pamoja na kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya elimu na ya biashara na masoko.[1]
Wasifu
haririAndy Chande alikuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shule ya Shaaban Robert Secondary School na rais wa chama cha ‘’Dar es Salaam Secondary Education Society’’. Pia alikuwa mdhamini wa heshima wa shule za jamii ya watu wenye asili ya Uhindi katika mkoa wa Dar es Salaam
Andy Chande amepokea tuzo mbalimbali: mwaka 1998 alipata tuzo kutoka Rotary International ilioitwa ‘’Service Above Self’’ na mwaka 2003 alipokea tuzo ya ‘’Hind Ratna’’ kutoka kwa Waziri Mkuu mstaafu wa India ikiwa ni tuzo ya heshima ya mtu wa mwaka asiyekuwa raia wa India.
Tarehe 10 Agosti 2007, kitabu chake A Knight in Africa” kilichotafsiriwa katika lugha ya Kiswahili kama Shujaa Katika Afrika: Safari Kutoka Bukene kilizinduliwa na rais wa awamu ya nne nchini Tanzania, Jakaya Kikwete katika ukumbi wa shule ya Shaaban Robert Secondary School, huku marais na watu wengine waliohudhuria siku hiyo akiwemo:
- Rais wa pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi
- Rais wa tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa
- Dr Andrew McAlister[1]
Tuzo
hariri- Knight Commander of the Most Excellent Order of the British Empire, 2003
- Pravasi Bharatiya Samman, 2005
Marejeo
hariri- ↑ "Prominent businessman Andy Chande dies at 88", The Citizen, 2017-04-07. (en)
Viungo vya Nje
hariri- [http:// Official website]
- A Knight in Africa Ilihifadhiwa 27 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Andy Chande kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |