Anyesi wa Montepulciano
Anyesi wa Montepulciano (Montepulciano, Toscana, Italia, 28 Januari 1268 - Montepulciano, 20 Aprili 1317) alikuwa bikira wa ukoo bora aliyejiweka wakfu akiwa na umri wa miaka 9. Alikuwa na vipaji na karama za pekee kiasi kwamba akiwa na umri wa miaka 15 tu alichaguliwa na kuthibitishwa kuwa abesi katika monasteri mpya ya Kifransisko.

Baadaye alikubali kurudi kwao alipoanzisha nyingine aliyoiunganisha na familia ya kiroho iliyoanzishwa na Dominiko Guzman ambaye alikuwa amemtokea kwa ajili hiyo[1][2].
Anyesi alitangazwa na Papa Benedikto XIII kuwa mtakatifu mwaka 1726[3].
Tazama pia Edit
Tanbihi Edit
- ↑ Dorcy, Marie Jean. St. Dominic's Family, Tan Books and Publishers, (1983). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-05-27. Iliwekwa mnamo 2021-04-16.
- ↑ Sant' Agnese Segni di Montepulciano (it). Santi Beati.
- ↑ (1996) Giambattista Tiepolo, 1696-1770 : [Venice, Museum of Ca' Rezzonico, from September 5 to December 9, 1996 : The Metropolitan Museum of Art, New York, [from January 24 to April 27, 1997]] (in en). Metropolitan Museum of Art, 222. ISBN 978-0-87099-812-6.
- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Vyanzo Edit
- Raimondo wa Capua, Sant'Agnese da Montepulciano, Cantagalli, Siena 1983.
Viungo vya nje Edit
- Fitzgerald, Edward Gregory (1907). "St. Agnes of Montepulciano". Catholic Encyclopedia. 1. New York: Robert Appleton Company.
- Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN|0-14-051312-4.
- "Saint Agnes of Montepulciano" at the Christian Iconography website
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |