Askari wafiadini wa Kapadokia

Askari wafiadini wa Kapadokia (walifariki karibu na Sivas, Armenia ya Kale, leo nchini Uturuki, 303) ni kundi la Wakristo 40 wa Kapadokia ambao waliuawa wakati wa dhuluma ya kaisari Licinius kwa sababu ya imani yao. Hawakuwa ndugu kwa asili, ila kwa kutimiza pamoja mapenzi ya Mungu.

Baada ya kufungwa na kuteswa sana, wakati wa baridi kali waliachwa usiku kucha uchi kwenye ziwa lililoganda na hatimaye walivunjwa miguu.

Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao inaadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Machi[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.