Dhahabu

(Elekezwa kutoka Auri)


Dhahabu (kutoka Kiarabu ذهب, dhahab) ni elementi yenye namba atomia 79 katika mfumo radidia na uzani atomia ni 196.966569. Alama yake ni Au (kutoka Kilatini aurum).

Dhahabu
Jina la Elementi Dhahabu
Alama Au
Namba atomia 79
Uzani atomia 106.42 u
Valensi 2, 8, 18, 32, 18, 1
Ugumu (Mohs) 2.5
Kiwango cha kuyeyuka 1337.33 K (1064.18 °C)
Kiwango cha kuchemka 3129 K (2856 °C)
Punje za dhahabu jinsi zinavyopatikana kwenye ardhi au mtoni.

Ni metali adimu nzito yenye rangi ya njano nyeupe hadi njano nyekundu. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 1337.33 K (1064.18 °C). Dhahabu haiathiriwi kwa urahisi kikemia: hii ndiyo sababu ya kung'aa kwa miaka mingi, kwa kuwa haishikwi na kutu.

Ni kati ya metali za kwanza kutumiwa na wanadamu. Sababu kubwa ni kwamba dhahabu hupatikana kama metali tupu. Atomu zake haziungani na elementi nyingi kuwa molekyuli ya dutu mpya, hivyo dhahabu haiozi kwa kushikwa na kutu. Ni elementi chache zinazoweza kuathiri dhahabu, hasa halojeni kadhaa. Rangi yake ni ya kuvutia na tabia yake ya kuchongeka baridi kwa kuponda tu kuwa bati au waya inawezesha watu kuipa maumbo tofauti. Ni metali laini, haifai kwa silaha au vifaa vya kazi lakini ilitumiwa tangu zamani kwa mapambo au kwa vyombo vya thamani katika utumishi wa kidini au wa kifalme.

Kwa sababu ya kuwa metali haba ilitumiwa kama pesa.

Upatikanaji wa dhahabu

hariri

Kwa wastani kuna takriban gramu 4 za dhahabu katika tani 1000 za miamba kwenye ganda la dunia. Hali halisi kiwango hicho ni tofauti sana kati ya mahali na mahali. Kiasi kikubwa cha dhahabu kinapatikana kwa umbo la vipande au zaidi chembe ndogo sana ndani ya mwamba au mashapo (ambayo ni miamba iliyovunjika na kuwa imara tena). Sehemu ndogo ya dhahabu hiyo kutoka miamba na ardhi imebebwa na maji ya mito; hapo ilizama chini kutokana na uzito wake na ilikandamizwa mara nyingi kuwa kama mawe madogo ya dhahabu (Kiingereza: nuggets) yaliyopatikana katika mito na kuwa chanzo cha dhahabu nyingi iliyopatikana katika historia.

Siku hizi dhahabu inatolewa katika migodi mikubwa ambako tani nyingi za ardhi au miamba yenye kiwango cha dhahabu cha kutosha zinachimbwa halafu dhahabu kutolewa kwa kutumia mbinu za kikemia.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dhahabu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.