Bahari ya Ross ni sehemu ya Bahari ya Kusini iliyopo katika hori kubwa huko Antaktiki kati ya Nchi ya Viktoria na Nchi ya Marie Byrd.

Ramani ya Bara la Antaktiki.

Maelezo hariri

Bahari ya Ross iligunduliwa na nahodha Mwingereza James Ross mnamo 1841. Magharibi mwa Bahari ya Ross kipo Kisiwa cha Ross. Mashariki kiko Kisiwa cha Roosevelt. Sehemu ya kusini imefunikwa na barafu. [1] Katika magharibi mwa bahari ya Ross kuna bandari ambayo kwa kawaida huwa haina barafu wakati wa kiangazi.

New Zealand inadai usimamizi juu ya maeneo yote katika Bahari ya Ross.

Umuhimu wa kiikolojia na uhifadhi hariri

Katika msimu wa joto kuna planktoni nyingi ambayo ni muhimu kama chanzo cha chakula kwa spishi kubwa kama vile samaki, sili, nyangumi, na ndege wa bahari.

Kwenye pwani za bahari hii kuna sehemu ambapo spishi mbalimbali za ngwini hukutana na kuzaa. [1]

Bahari ya Ross ni mojawapo ya sehemu za mwisho za bahari duniani zisizoathiriwa bado na shughuli za wanadamu. Kwa sababu hiyo hakuna uchafuzi wa mazingira.

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: