Bahari ya Tasmania

Bahari ya Tasmania ni bahari ya pembeni ya Pasifiki Kusini iliyopo kati ya Australia, Kisiwa cha Tasmania na New Zealand. Eneo lake ni takriban kilomita za mraba 2,331,000 likiwa na upana wa km 2,000 na urefu wa km 2,800. Maji yake hufikia kina cha mita 5,200.

Eneo la Bahari ya Tasmania.
Ramani ya Bahari ya Tasmania.

Jina la bahari pamoja na kisiwa cha Tasmania limetokana na nahodha Mholanzi Abel Tasman, aliyekuwa Mzungu wa kwanza kupita huko na kuchora ramani mnamo mwaka 1642/1643. Mwingereza James Cook alifuata mnamo 1770 akakazia utafiti wa eneo. [1]

Kujisomea hariri

  • Rotschi, H.; Lemasson, L. (1967), Oceanography of the Coral and Tasman Seas (PDF), Oceanogr Marine Biol Ann Rev, ASIN B00KJ0X6D4

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  1. "Tasman Sea". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 3 January 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)