Uholanzi
| |||||
Hadabu ya Taifa: Je maintiendrai (Kifaransa) kwa Kiswahili, Nitastahimili | |||||
Lugha za Taifa |
Kiholanzi kwa mkoa wa Friesland: Kifrisi | ||||
Mji Mkuu | Amsterdam | ||||
Makao ya Serikali | Den Haag | ||||
Mfalme | Koning Willem-Alexander | ||||
Waziri Mkuu | Mark Rutte | ||||
Eneo - Jumla - % Maji |
41,526 km² 18.41 | ||||
Umma - Jumla - msongamano |
16,856,620 (Julai 2014) 406.4/km² | ||||
GDP - Jumla - kwa kipimo cha umma |
$625 bilioni $ 30,500 | ||||
Uhuru - Tangazwa - Kukubaliwa |
Kutoka Hispania 26 Julai 1581 30 Januari 1648 | ||||
Fedha | Euro € EUR | ||||
Saa za Eneo | UTC +1 | ||||
Wimbo wa Taifa | Wilhelmus | ||||
TLD mtandao | .nl | ||||
Kodi ya simu | 31 |
Uholanzi ni nchi ya Ulaya ya Magharibi. Imepakana na Ujerumani upande wa mashariki, Ubelgiji upande wa kusini na Bahari ya Kaskazini (North Sea) upande wa magharibi na kaskazini.
Uholanzi ni sehemu ya "Ufalme wa Nchi za Chini" (Kingdom of the Netherlands) pamoja na visiwa vya Aruba, Curaçao na Sint Maarten, mbali ya visiwa vingine vitatu vya Karibi vya Uholanzi.
Jina la Uholanzi limetokana na “Holland”, eneo la magharibi la nchi hii. Watu wengi hutumia jina hilo, lakini wakazi wenyewe wanaiita nchi yao “Nederland” inayomaanisha "nchi ya chini". Kwa kweli, sehemu kubwa ya Uholanzi iko chini ya usawa wa bahari. Waholanzi wamejenga maboma kuzuia maji yasienee yakifurika.
Jiografia
haririAkifika Uholanzi kwa uwanja wa ndege wa Schiphol, msafiri anastaajabu nchi ilivyo tambarare. Kwa kweli, kuna sehemu zenye vilima, lakini sehemu kubwa zaidi ya Uholanzi ni tambarare.
Mahali pa juu kabisa nchini ni Kilima cha Vaals, upande wa kusini wa mkoa wa Limburg, kwa 322 m. Mahali pa chini kabisa ni karibu na Nieuwerkerk aan de IJssel, mkoa wa Zuid Holland, kwa -6.76 m (mita 6.76 chini ya usawa wa wastani wa bahari).
Vipande vikubwa vya nchi vimepatikana kutoka ziwa au bahari. Ili kufanya hivyo boma linajengwa kuzunguka ziwa au sehemu ya bahari, kisha maji yanavutwa kwa bomba. Mahali kati ya boma huitwa “polder”. Mkoa mmoja mzima, Flevoland, umepatwa kwa maji ya “Zuiderzee” (Bahari ya Kusini). Kwa sababu hiyo watu husema: “Mungu aliumba dunia lakini Waholanzi waliumba Uholanzi.” Hata sasa sehemu muhimu ya Uholanzi ni maji: 18%.
Maboma mengine makubwa yamejengwa upande wa kusini magharibi wa nchi ili ya kuzuia maji yasienee mikoa ya Zeeland na Zuid Holland. Mradi huu huitwa “Deltawerken” au Ujenzi wa Delta. “Oosterscheldekering” au boma la mto wa Oosterschelde ni jengo linaloshangaza. Urefu wake ni 9 km na katikati yake kuna malango makubwa 62 ambayo hujifunga wenyewe kila wakati ambapo maji ya bahari yakifura zaidi ya 3 m. Barabara kuu inapitia juu ya boma hili.
Mito
haririMito mikubwa kadhaa inaingia Uholanzi na kutiririka katika Bahari ya Kaskazini. Mto Rijn (Mto Rhine) unaingia kwa Tolkamer upande wa mashiriki, na karibu na Nijmegen Mto Waal unajitenga ambao unachukua 70% ya maji. Mto IJssel unajitenga karibu na Westervoort na kwenda upande wa kaskazini. Mto Maas (Mto Meuse) unaingia Uholanzi upande wa kusini wa Limburg, na karibu na Mook unageuka upande wa magharibi. Mto Schelde unaingia upande wa kusini wa Zeeland.
Mikoa
haririUholanzi umegawanyika katika mikoa 12. Kila mkoa unatawaliwa na gavana ambaye huitwa “Commissaris van de Koningin” isipokuwa yule wa Limburg ambaye huitwa “Gouverneur”. Mikoa na miji mikuu yao ni :
Mkoa | Mji mkuu |
---|---|
Groningen | Groningen |
Friesland | Leeuwarden |
Drenthe | Assen |
Overijssel | Zwolle |
Gelderland | Arnhem |
Utrecht | Utrecht |
Flevoland | Lelystad |
Noord-Holland | Haarlem |
Zuid-Holland | Den Haag (The Hague) |
Zeeland | Middelburg |
Noord-Brabant | ’s-Hertogenbosch (Den Bosch) |
Limburg | Maastricht |
Miji mikubwa
haririMji | Wakazi |
---|---|
Amsterdam | 742,011 |
Rotterdam | 600,000 |
Den Haag | 476,000 |
Utrecht | 281,569 |
Eindhoven | 209,399 |
Trafiki
haririKatika Uholanzi barabara daima zina msongamano wa magari. Hii ni kwa sababu watu wanakwenda kazini asubuhi hadi kurejea jioni, na wanaoishi Uholanzi ni wengi, na kufanya kazi nyingi sana.
Historia
haririKisha kutekwa na Julius Caesar katika karne ya 1 KK, kusini mwa nchi ikawa mpaka wa kaskazini wa Dola la Roma hadi lilipokoma (karne ya 5).
Baadaye nchi ilivamiwa na makabila mbalimbali ya Wagermanik: Wasaksoni, Wabatavi, Wafrisi na Wafaranki.
Katika karne ya 8 nchi ilikuwa sehemu ya dola la Karolo Mkuu, na katika karne ya 10 ya Dola Takatifu la Kiroma.
Baadaye mfumo wa ukabaila ulitawala nchi sehemu sehemu.
Katika karne ya 16 nchi ilikuwa chini ya familia ya makaisari (Absburg), lakini ilipokea Matengezo ya Kiprotestanti kinyume cha matakwa ya kaisari Karolo V.
Mwanae Filipo II wa Hispania alipomrithi hakukubali jambo hilo na kusababisha uasi ulioenea kote (1566-1581) hadi wilaya saba zilipounda jamhuri iliyotambuliwa na Hispania mwaka 1648 tu, katika amani ya Westfalia.
Karne ya 17 ndipo nchi ilipofikia kilele cha ustawi wake, ikiwa na makoloni mengi huko India, Indonesia, Afrika na Amerika, pamoja na biashara kubwa ya kimataifa duniani kote.
Karne iliyofuata Uingereza ulishika nafasi hiyo ya Uholanzi.
Baada ya mapinduzi ya Kifaransa (1789) nchi ilitekwa na Wafaransa hadi Amani ya Vienna (1814-1815) iliyopanua Uholanzi huru tena, lakini kwa mfumo wa ufalme.
Hata hivyo mwaka 1830 Ubelgiji ulijitenga na mwaka 1890 Luxemburg ilifanya vilevile.
Uholanzi haukutaka kushiriki Vita vikuu vya kwanza vya dunia, lakini katika vita vikuu vya pili ulivamiwa na Ujerumani (1940-1945).
Baadaye Uholanzi umejitahidi sana kushiriki katika mahusiano ya kimataifa na ni kati ya nchi waanzilishi wa Umoja wa Ulaya.
Watu
haririWakazi wengi wana asili ya makabila ya Kijerumani, lakini kuna wahamiaji wengi pia kutoka nchi nyingi. 22% za wakazi wana walau mzazi mmoja kutoka nchi za nje.
Lugha ya kawaida ni Kiholanzi.
Upande wa dini, takwimu za serikali zinaonyesha kwamba mwaka 2015, 50.1% ya wakazi hawakuwa na dini yoyote, 43.8% walikuwa Wakristo (23.7% Wakatoliki, 21.1% Waprotestanti, hasa Wakalvini, 4.9% Waislamu, 1.1% Mabanyani, Wabuddha n.k.
Tazama pia
haririViungo vya nje
haririHistoria, jiografia na siasa
hariri- Overheid.nl Ilihifadhiwa 26 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine. - Lango rasmi la serikali ya Uholanzi
- Ramani na takwimu
- Mikoa ya Uholanzi
- CBS Ilihifadhiwa 30 Machi 2016 kwenye Wayback Machine. - Takwimu rasmi
- Makala ya Encarta kuhusu Uholanzi Ilihifadhiwa 16 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
- Government.nl - Tovuti rasmi ya serikali ya Uholanzi
- CIA - The World Factbook -- Netherlands Ilihifadhiwa 9 Mei 2007 kwenye Wayback Machine.
- Habari za Uholanzi: Radio Netherlands Ilihifadhiwa 29 Aprili 2010 kwenye Wayback Machine. - Redio ya Uholanzi kwa lugha ya Kiingereza
Kusafiri
hariri- Netherlands travel guide kutoka Wikisafiri
- World66's guide to the Netherlands Ilihifadhiwa 13 Mei 2006 kwenye Wayback Machine. - Kiongozi cha kusafiri kinachoandikwa na watumiaji.
- Kiongozi cha kusafiri katika Uholanzi Ilihifadhiwa 15 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
- Picha za Uholanzi Ilihifadhiwa 28 Oktoba 2016 kwenye Wayback Machine.
- Just Landed Netherlands - Habari za manufaa kwa kuhamia Uholanzi
Viungo anuwai
hariri- Ujenzi wa Delta kwa mtandao
- Keukenhof Bustani za Maua Ilihifadhiwa 4 Mei 2006 kwenye Wayback Machine. - Picha nzuri mno za bustani za maua katika Uholanzi.
- Familia ya kifalme ya Uholanzi Ilihifadhiwa 2 Februari 2010 kwenye Wayback Machine.
- Kiholanzi kwa wasemao Kiingereza
- Orodha ya majengo marefu 1500 katika Uholanzi Ilihifadhiwa 8 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uholanzi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |