Mpira wa kikapu

(Elekezwa kutoka Basketball)

Mpira wa kikapu ni aina ya michezo inayopendwa katika sehemu nyingi za dunia na watu wengi hutamani mchezo huu.

Mpira wa kikapu.

Mara nyingi hufanywa ukumbini wakati timu mbili za wachezaji wanajaribu kuingiza mpira katika kikapu cha timu nyingine.

Vikapu viko mwishoni mwa upande mwembamba wa uwanja kwa urefu wa mita 3.05.

Kila timu huwa na wachezaji 5 uwanjani na hadi wachezaji wa kando 7 walio tayari kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine muda wowote.

Kila goli katika kikapu cha upande mwingine linahesabiwa kama pointi 2 au 3, kutegemeana na umbali wa kurusha. Goli la penati huleta pointi 1 tu.

Historia hariri

Mchezo huu ulianzishwa na mwalimu James Naismith kwenye chuo cha Springfield College huko Massachusetts mwaka 1891Alibuni mchezo huo kwa ajili ya wanafunzi wake ili wapate mazoezi wakati wa kipupwe waliposhindwa kucheza nje.

Mpira wa kikapu ulienea haraka kwenye vyuo vya Marekani, na katika karne ya 20 pia nje ya vyuo.

Mwaka 1936 mchezo huu ulikubaliwa kwenye michezo ya olimpiki.

Hadi leo ligi muhimu zaidi duniani ni ile ya Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani.

 
Vipimo vya uwanja wa mpira wa kikapu

Kanuni za mpira wa kikapu hariri

Shabaha ya mchezo ni kushinda vikapu vingi kuliko timu nyingine.

Mpira unaotumiwa kimataifa ni mpira wa ngozi au mata sintetiki wenye kipenyo cha milimita 749 hadi 780 na uzito wa gramu 567 hadi 650.

Uwanja huwa na vipimo vya mita 28 kwa 15.

Wakati wa mchezo kuna marefa 2-3 uwanjani. Kando ya uwanja hukaa waamuzi wengine wanaoshika wakati na miniti za magoli na makosa.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • FIBA Archived 4 Novemba 1996 at the Wayback Machine., Fédération Internationale de Basketball / International Basketball Federation
  • IWBF, International Wheelchair Basketball Federation
 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Mpira wa kikapu kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.