Brandi

(Elekezwa kutoka Brandy)

Brandi (kutoka Kiingereza: brandy) ni kinywaji cha alikoholi kilichotengenezwa kutokana na zabibu au pia matunda mengine.

Bilauri ya Brandi

Rangi na ukali

hariri

Kuna aina nyingi, kwa kawaida huuzwa ikiwa na viwango vya alikoholi kati ya asilimia 35- 60.[1]

Rangi yake ni kama maji au kahawia. Asili yake ni kukeneka kwa divai au juisi ya matunda iliyochachuka.

Pale inapotoka kwenye chombo cha kukeneka haina rangi sawa na maji. Lakini aina mbalimbali huiva katika mapipa ya mbao na hapo rangi hubadilika kuwa ya kikahawia.

Brandi ya divai

hariri

Kufuatana na sheria za Umoja wa Ulaya "brandy" inapaswa kutengenezwa kutoka divai pekee ikiiva baadaye katika mapipa ya mbao. Inaruhusiwa kuongeza sukari. Aina mashuhuri za brandi za divai ni kama vile Cognac (tamka kon-yak, ni asili ya jina la Kiswahili konyagi) na Armagnac kutoka Ufaransa, Brandy de Jerez kutoka Hispania.

Nchi zote zinazotengeneza divai zinajua pia brandi zinazopatikana kwa kutumia maganda ya zabibu yaliyoondolewa juisi tayari ilhali mabaki bado yapo; mabaki hayo huongezewa maji na kuchachua, matokeo hukenekwa. Grappa ya Italia hupatikana kwa njia hiyo.

Katika nchi za Mashariki ya kati brandi ya divai au maganda ya divai huongezewa ladha hasa kwa kutumia mbegu za pimpinella anisum (aniseed) na hii inaleta Ouzo ya Ugiriki, Raki ya Uturuki na Arrak ya Waarabu.

Brandi ya matunda

hariri

Kimsingi inawezekana kutumia matunda yoyote kwa brandi ya matunda kwa ukenekaji wa brandi, ama kwa kutoa juisi au kusaga tunda lote halafu kuichachua, kama kiwango cha sukari ndani ya tunda kinatosha.

Watumiaji hupenda ladhaa maalum inayotokana na kila tunda.

Marejeo

hariri
  1. "The History of Brandy".
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Brandi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.