Bungo mpenda-giza
Bungo wa unga (Tenebrio molitor)
Bungo wa unga (Tenebrio molitor)
Mnyoo wa unga (Tenebrio molitor)
Mnyoo wa unga (Tenebrio molitor)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Coleoptera (Wadudu wenye mabawa magumu)
Nusuoda: Polyphaga
Familia ya juu: Tenebrionoidea
Familia: Tenebrionidae
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Nusufamilia 11:

Bungo wapenda-giza au madundu ni mbawakawa wa familia Tenebrionidae katika nusuoda Polyphaga ya oda Coleoptera. Kama bungo wote wanaweza kuwa wakubwa lakini wadogo pia. Baadhi ya spishi zinaweza kuwa haribifu, kama vile bungo wa unga (inayojulikana zaidi kama mnyoo wa unga). Kuna spishi zaidi ya 20,000 duniani kote; idadi ya spishi za Afrika ya Mashariki haijahesabiwa.

Maelezo

hariri

Kwa ujumla, mbawakawa hawa wanafanana sana na mbawakawa wa wastani. Katika ukaguzi wa karibu, sifa zifuatazo zinaweza kutambuliwa:

Lava ni ndefu, nyembamba na ya umbo la mcheduara na wana kutikulo yenye siklerotini nyingi. Kwa kawaida huwa na rangi ya manjano hadi rangi ya machungwa isiyoiva.

Biolojia na ekolojia

hariri

Kama jina lao linavyoonyesha, wapevu hupenda kukaa mahali penye giza kama vile chini ya takataka au mawe, kwenye nyufa na mashimo. Wapevu na lava wa spishi nyingi ni wakulavyote wanaokula majani yanayooza, ubao unaooza, dutu bichi ya mimea, wadudu waliokufa na kuvu. [10] Wengine wamebobea katika kula nyoga. Spishi nyingi kubwa zaidi haziruki, mara nyingi kwa sababu mabawa yao mangumu ya mbele yameunganishwa pamoja, haswa katika maeneo makavu, ili kupunguza uvukizaji. Wapevu wa spishi nyingi huishi muda mrefu zaidi kuliko wadudu wengine wengi, kama miezi sita hadi miaka miwili.

Lava wanaoishi ardhini huitwa nyunguwaya bandia (nyunguwaya wa kweli ni lava za bungo-fyatuo). Wanakula dutu za kikaboni zinazooza lakini pia wanaweza kusababisha hasara kwa kula mbegu zinazoota na kutafuna mizizi na machipukizi ya miche. Mara nyingi wao ni chanzo kinono cha chakula cha ndege na mamalia wadogo. Lava wengine hula nafaka iliyohifadhiwa na bidhaa zingine kama unga, nafaka za kiamshakinywa, tambi, biskuti, maharagwe na makokwa. Hawa huitwa minyoo ya unga, ikiwa ni pamoja na wale wa bungo mwekundu wa unga (Tribolium castaneum).

Bungo wapenda-giza ni sehemu muhimu ya kina wadudu wa jangwani pamoja na bungo-mavi. Wale walio katika Jangwa la Namib wamebadilika kwa njia ambayo hukusanya matone ya ukungu yanayowekwa kwenye mabawa yao. Matone yanapokusanyika, maji hutiririka chini ya mgongo wa bungo hadi kwenye sehemu za kinywa, ambapo yanamezwa.[14]

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Orientochile elegans
  • Pycnocerus passerini
  • Strongylium mirabile
  • Tenebrio giganteus
  • Tenebrio molitor
  • Tribolium castaneum