Cyangugu
Cyangugu (awali: Shangugu) ni mji ulioko magharibi mwa Rwanda. Unaundwa na Cyangugu yenyewe na Kamembe.
Majiranukta: 2°29′00″S 28°55′00″E / 2.48333°S 28.91667°E | |
Nchi | Rwanda |
---|---|
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 63.883 |
Ndiyo makao makuu ya wilaya ya Rusizi. Mto Ruzizi unatenganisha mji huo na mji wa Bukavu ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kamembe
haririKamembe ni moja ya sehemu mbili zinazounda mji huo ulioko magharibi mwa Rwanda kwenye umbali wa karibu km 250 (maili 155) kutoka mji mkuu wa Rwanda, Kigali. Hakuna umbali kati ya Kamembe na mpaka wa Jamhuri ya Burundi.
Kamembe ni mmoja kati ya miji ya Rwanda ambako ziwa Kivu linapatikana.
Mji wa Kamembe una uwanja wa ndege ulio wa pili kwa ukubwa nchini Rwanda. Kupeana kwake mpaka na Bukavu, DRC na kukaa kwake karibu na Burundi kuliwavutiya wahamiaji wengi kutoka nchi hizi zote mbili ambao walifanya Kamembe kuwa makazi yao ya kudumu.
Wahamiaji wengine waliokuwa Kamembe walikuwa Waarabu ambao walikuja na kukaa Kamembe aidha kama vile wakimbizi wa vita vilivyowahi kutokea huko visiwa vya Unguja au wafanyabiashara waliojihusisha na biashara ya bidhaa kama vile kahawa na ngozi wa ng'ombe. Biashara ya bidhaa hizo ilishamiri sana katika miaka ya 1930 hadi mwishoni mwa miaka ya 1970.
Mchanganyiko huo wa raia kutoka nchi jirani, uhamiaji wa Waarabu na kushamiri kwa biashara ya bidhaa hizo, kulifanya Kamembe kuwa na hali ya pekee ukilinganisha na miji mingine ya nchini Rwanda.
Hali ya pekee kubwa ya mji wa Kamembe ni matumizi ya lugha ya Kiswahili. Tofauti na kwingineko kote Rwanda ambako lugha inayotumika ni lugha ya taifa ya Rwanda, yaani Kinyarwanda, Kamembe ndiko utumiaji wa lugha ya Kiswahili ulizagaa kwa vikubwa.
Tofauti nyingine ni kuenea sana kwa dini ya Uislamu. Ukilinganisha na kwingineko Rwanda, ambako dini kubwa ni Ukristo wa madhehebu ya Uprotestanti na Ukatoliki, zaidi ya asilimia 95 za wakaaji wa mji wa Kamembe ni Waislamu. Utumiaji wa Kiswahili na kujiri kwa dini hiyo vilifanya Kamembe kutofautiana kabisa na mahala pengine nchini Rwanda, kimila na kiutamaduni.
Huku kulifanya wanasiasa waliyoitawala Rwanda kabla ya serikali ya sasa iliyoko nchini Rwanda kuwashika raia wa Kamembe kama vile raia wasio wa Rwanda. Kwa serikali hizo raia wa Kamembe waliitwa Waswahili. Hii ilisababisha wanyimwe haki zao mbalimbali za kiraia. Japo kuwa haya yalibadilika wakati serikali ya sasa ikiongozwa na RPF iliingia madarakani nchini Rwanda mnamo mwaka wa 1994.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Cyangugu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |