Danubi (mto)

(Elekezwa kutoka Danube)

Danubi ni mto mrefu wa pili katika Ulaya baada ya Volga.

Mto wa Danubi
Mto wa Danubi huko Budapest (Hungaria)
Mto wa Danubi huko Budapest (Hungaria)
Chanzo Milima ya Msitu Mweusi, Ujerumani
Mdomo Bahari Nyeusi
Nchi za beseni ya mto Romania (28.9%), Hungaria (11.7%), Austria (10.3%), Serbia (10.3%), Ujerumani (7.5%), Slovakia (5.8%), Bulgaria (5.2%), Bosnia na Herzegovina (4.8%), Kroatia (4.5%), Ukraine (3.8%), Ucheki (2.6%), Slovenia (2.2%), Moldova (1.7%), Uswisi (0.32%), Italia (0.15%), Poland (0.09%), Albania (0.03%)
Urefu 2,857 km
Kimo cha chanzo 1,087 m
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni 6,500 m³/s
Eneo la beseni (km²) 801,463 km²
Ramani ya Danubi

Jina lina asili katika lugha za Kislanovi na kumaanisha kiasili "mto". Mto huu unapita katika nchi nyingi na majina yake ni Donau (Kijerumani), Dunărea (Kiromania), Dunav (Kikroatia na Kiserbia), Duna (Kihungaria) na Dunaj kwa Kislovakia.

Chanzo na mwendo hariri

Danubi inaanza Ujerumani ambako mito midogo ya Brigach na Breg inakutana karibu na mji Donaueschingen katika eneo la Msitu Mweusi. Danubi inaishia Romania katika delta yake kwenye Bahari Nyeusi.

Mto wa nchi kumi hariri

Danubi ni mto wa nchi kumi. Kwenye 1070 km (37 %) za mwendo wake mto ni mpaka wa nchi fulani. Mto haupiti hata kidogo ndani ya Kroatia, Bulgaria, Ukraine na Moldova lakini ni mstari wa mpaka wa nchi hizi zinagusana na Danubi tu ukingoni wa mto upande mmoja. Inapita katika nchi zifuatazo au kugusa mipaka yao:

Nchi kwenye Danubi
  Kilomita
za mto nchini
au mpakani
Ukingo wa mto
upande wa kulia
Kingo zote mbili Ukingo wa mto
upande wa kushoto
Nchi - jina la mto nchini km % km % km %
Ujerumani - Donau 687,00 658,6 23 658,6 36 687,0 24
Austria - Donau 357,50 357,5 12 321,5 18 321,5 11
Slovakia - Dunaj
tamka: dunay
172,06 22,5 1 22,5 1 172,1 6
Hungaria - Duna 417,20 417,2 14 275,2 15 275,2 10
Kroatia - Dunav 137,50 137,5 5 0,0 0 0,0 0
Serbia - Дунав / Dunav 587,35 449,9 16 220,5 12 358,0 12
Romania - Dunăre 1075,00 374,1 13 319,6 18 1020,5 35
Bulgaria - Дунав (Dunav) 471,55 471,6 16 0,0 0 0,0 0
Moldova - Dunare 0,57 0,0 0 0,0 0 0,6 0
Ukraine - Дунай (Dunay) 53,94 0,0 0 0,0 0 53,9 2

Namba za asilimia zinahusu urefu wa mto wote na sehemu ya kila nchi (Rejeo: Kamati ya kimatifa ya Danubi, Budapest, Januari 2000-Machi 2004)

Picha hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Danubi (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.