Defendente (kwa Kilatini: Defendens; alifariki 286-287 hivi) alikuwa askari wa kikosi cha Thebe katika jeshi la Roma ya Kale aliyeuawa wakati wa dhuluma ya kaisari Maksimiani dhidi ya Wakristo.

Mt. Defendente alivyochorwa katika kanisa la Clusone.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Januari.

Kifodini chake

hariri

Kufuatana na mapokeo ya karne ya 4 kikosi hicho, kilichoongozwa na Morisi, kilijumlisha wanajeshi Waafrika elfu moja kutoka Misri ya kusini na Nubia waliotumwa Ulaya wakati wa Kaisari Maximiano wa Roma. Wengi wao walikuwa Wakristo.

Huko Agaunum, karibu na mto Rhone, katika eneo la Uswisi wa leo, walipewa amri ya kujiandaa kwa mapigano dhidi ya waasi na kabla ya mapigano kutoa sadaka kwa Kaisari aliyeheshimiwa kama mungu mmojawapo. Wakristo hao walikataa kutoa sadaka hiyo. Kaisari alipopata habari hii akakasirika akatoa amri kuua kila askari wa kumi katika kikosi. Wakristo walipoendelea kukataa amri ilirudiwa hatimaye karibu kikosi chote kiliuawa pamoja na kiongozi chake Morisi.

Heshima baada ya kifo

hariri

Morisi pamoja na askari wa kikosi cha Thebi waliheshimiwa kama watakatifu na wafiadini Wakristo.

Katika mapokeo ya sanaa ya Kikristo walichorwa kama Waafrika weusi.

Miji mbalimbali ya Uswisi na Ujerumani walitumia na wanatumia picha za Morisi au watakatifu wengine wa Kikosi cha Thebi katika nembo zao. Mara nyingi kama mji wa Ulaya una picha ya mtu mweusi katika nembo yake hii inammaanisha Morisi Mtakatifu au wenzake.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.