Dominiko Loricatus

Dominiko Loricatus, O.S.B. Cam. (kwa Kiitalia: San Domenico Loricato; 995 - 1060), alikuwa mmonaki wa Italia mzaliwa wa kijiji cha Luceolis karibu Cantiano (leo katika mkoa wa Marche).

Mt. Dominiko Loricatus kadiri ya M. de Vos.

Baba yake, akitamani maendeleo, alitoa rushwa ili huyo mwanae mdogo apewe upadrisho. Dominiko alipopata habari aliamua kufanya toba kama mkaapweke.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Oktoba.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit