Dorotheo wa Turo (Antiokia ya Siria, leo nchini Uturuki, 255 hivi - Varna, Bulgaria, 362) alikuwa askofu wa mji huo wa Lebanoni [1].

Mchoro mdogo kutoka Menologion ya Basili II.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Juni[2][3].

Maisha hariri

Dhuluma ya kaisari Diocletian ilimlazimisha kukimbia alipokuwa padri maarufu kwa elimu yake, lakini baadaye akarudi.

Alishiriki mtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka 325, lakini alifukuzwa na kaisari Juliani Mwasi akakae Odyssopolis (Varna, leo nchini Bulgaria) kwenye Bahari Nyeusi. Huko alifia dini yake akiwa na umri wa miaka 107[4].

Maandishi hariri

Anasemekana kuwa mwandishi wa kitabu "Matendo ya Wanafunzi Sabini" waliotumwa na Yesu kadiri ya Injili ya Luka 10:1.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Eusebius,VII.32
  2. Martyrologium Romanum
  3. Saint Dorotheus of Tyre. Saints.SQPN. Iliwekwa mnamo April 5, 2011.
  4. https://www.santiebeati.it/dettaglio/93025

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.