Edmond Halley (8 Novemba 1656 - 14 Januari 1742) alikuwa mwanaastronomia kutoka nchini Uingereza. [1]

Edmond Halley mnamo 1690.
Halley mzee, mnamo 1736.
Kaburi la Halley.

Alikuwa pia mtaalamu wa hisabati, wa metorolojia na wa fizikia. Halley anajulikana zaidi kwa kukadiria obiti ya nyotamkia iliyopata jina lake, yaani Nyotamkia ya Halley .

Familia na elimu ya awali

hariri

Halley alizaliwa katika kaunti ya Middlesex, Uingereza. Babake Edmond Halley alikuwa fundi wa sabuni mjini London na tajiri. Aliposoma shuleni kijana Halley alivutwa sana na hisabati. Alisoma shule ya St Paul's alipoanza kujifunza astronomia. 1673 aliingia Queen's College mjini Oxford. Wakati bado alikuwa mwanafunzi, Halley alitunga makala kuhusu Mfumo wa Jua na madoa ya Jua.

Pale Oxford Halley alifahamiana na mwanaastronomia mashuhuri John Flamsteed aliyekuwa akikusanya habari za nyota zote zilizoweza kutazamiwa kwenye angakaskazi na kuandaa orodha ya namba za Flamsteed. Halley alijitolea kufanya kazi ileile kwa ajili ya angakusi.

Kazi ya kitaalamu

hariri

Mnamo mwaka 1676, alipokuwa na umri wa miaka 20, aliondoka katika Oxford akasafiri kwenda kisiwa cha St Helena katika Atlantiki ya kusini akaanzisha paoneaanga na kuchunguza nyota akaweza kuorodhesha nyota 341 za angakusi. [2] Mafanikio haya yalimpatia shahada ya uzamili (MA).

Kwenye Septemba 1682 alitazama nyota yenye mendo kwenye aliyotambua kuwa ni nyotamkia ailiyowahi kutazamiwa. Alitabiri kurudi kwake mnamo mwaka 1758. Halley mwenyewe aliaga dunia kabla ya marudio lakini wataalamu wa wakati walikumbuka utabiri wake n hivyo nyotamkia hii iliyoendelea kurudi ilipata jina lake.

Mnamo 1686, Halley alichapisha sehemu ya pili ya matokeo kutoka kwa msafara wake wa St. Helena . Hii ilikuwa makala kuhusu upepo na monsuni. Hapa alitambua ni joto la Jua linalosababisha miendo katika angahewa. Aliatambua uhusiano baina kanieneo angahewa jinsi inavyopinwa kwa barometa na kimo juu ya usawa wa bahari . Halley pia alimshawishi Sir Isaac Newton kuchapisha kitabu kuhusu uvumbuzi wake wa graviti .

Mnamo 1691 Halley alitafuta nafasi ya Profesa wa astronomia katika Chuo Kikuu cha Oxford . Kwa vile alikuwa anajulikana kama mkanaji Mungu, alipingwa na Askofu Mkuu wa Canterbury, John Tillotson halafu hakuchaguiwa. [3]

Yaliyopewa jina la Halley

hariri
  • Kasoko ya Halley (kasoko kwenye Mwezi)
  • Kasoko ya Halley (kasoko kwenye sayari Mirihi)
  • Kituo cha Utafiti cha Halley, Antaktiki
  • Mbinu wa Halley, katika hisabati njia ya suluhisho la milinganyo mingi
  • Halley Street, huko Blackburn, Victoria, Australia Edmund Halley Road, mjini Oxford, Uingereza Nyotamkoa ya Halley, inayorudi kila baada ya miaka 76
  • Halley Street, huko Blackburn, Victoria, Australia
  • Edmund Halley Road, mjini Oxford, Uingereza
  • Nyotamkia ya Halley, inayorudi kila baada ya miaka 76

Marejeo

hariri
  1. Mra nyingi anatajwa kwa umbo la "Edmund" lakini mwenyewe alipendelea kuandika "Edmond" The Times (London) Notes and Queries #254, 8 November 1902 p36
  2. "Gazetteer - p7. Monuments in France - page 338". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-16. Iliwekwa mnamo 2019-10-15.
  3. Derek Gjertsen The Newton Handbook, p250.

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: