Eligius wa Noyon

(Elekezwa kutoka Eliji wa Noyon)

Eligius wa Noyon (kwa Kifaransa: Éloi; Chaptelat, Aquitaine, 588 hivi – Noyon, 1 Desemba 660) alikuwa sonara halafu mshauri mkuu wa mfalme wa Ufaransa Dagobati I, akichangia ujenzi wa monasteri nyingi na maziara mazuri ya kisanaa kwa heshima ya watakatifu.

Mt. Eliji alivyochorwa mwaka 1508.
Saini ya Mt. Eligius.

Miaka mitatu baada ya kifo cha mfalme huyo, alichaguliwa kuwa askofu wa Noyon-Tournai (642). Hapo kwa miaka ishirini alijitahidi kwa ari kufanya wakazi Wapagani wa Flandria waongokee Ukristo[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi[2] kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Desemba[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/80000
  2. December 1. Latin Saints of the Orthodox Patriarchate of Rome.
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.