Open main menu

Felisi wa Como (alifariki tarehe 8 Oktoba 391 BK) anakumbukwa kama askofu wa kwanza wa Como (Italia Kaskazini).

Rafiki wa Ambrosi wa Milano, alisifiwa naye kwa umisionari wake akapewa naye upadrisho mwaka 379[1]na daraja ya uaskofu kwa ajili ya Como tarehe 1 Novemba 386[2] katika juhudi za kukamilisha uenezi wa Ukristo kote Italia baada ya Kaisari Theodosi I kuufanya dini rasmi ya Dola la Roma.

Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake au tarehe 1 Julai.[3]

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit