Felisi wa Nicosia
Felisi wa Nicosia, O.F.M.Cap. (jina la awali Filippo Giacomo Amoroso) alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka Sicilia, leo nchini Italia (5 Novemba 1715 – 31 Mei 1787).
Baada ya kukataliwa miaka 10, alipopokewa utawani alitoa kwa unyofu na usafi wa moyo huduma duni alizoagizwa.
Ni maarufu hasa kwa utiifu wake wa ajabu, uliothibitishwa na kiongozi aliyejichukulia jukumu la kumjaribu na kumdhalilisha kwa kila namna.[1]
Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 12 Februari 1888, halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 23 Oktoba 2005.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-10. Iliwekwa mnamo 2014-10-05.
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |