Felisi wa Thibiuca

Felisi wa Thibiuca (247 hivi - 303 hivi) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji wa Thibiuca (leo Tubzak nchini Tunisia).

Aliuawa mjini Karthago (labda pamoja na Audactus, Fortunatus, Januarius na Septimus)) katika dhuluma ya kaisari Diokletian wa Dola la Roma, kwa kukataa amri ya kuchoma moto vitabu vitakatifu vya Biblia, akisema afadhali ajichome. Kwa hiyo aliuawa na liwali Anulino kwa upanga[1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Julai[2][3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.