Fransisko wa Meako

Fransisko wa Meako alikuwa Mkristo wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko aliyefia dini nchini Japani (1597).

Dhuluma dhidi ya Wakatoliki zilipozidi, yeye na wenzake 25 (mapadri na watawa 8 na walei 17[1]) walikamatwa, walitukanwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597, huku wakifurahia neema ya kuuawa namna ileile ya Yesu.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake na ya wafiadini wenzake huadhimishwa kila mwaka tarehe 6 Februari[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.