Yakobo Kisai
Yakobo Kisai (takriban 1533 – 5 Februari 1597) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki nchini Japani.
Ametambuliwa kuwa mtakatifu kama mfiadini.
Sikukuu yake ni tarehe 6 Februari[1].
Maisha
haririAlizaliwa nchini Japani na baada ya kuachwa na mke wake alijiunga na Shirika la Yesu (Wajesuiti), akahubiri Injili kwa ufanisi.
Lakini dhuluma dhidi ya Wakatoliki zilipozidi, yeye na wenzake 25 (mapadri na watawa 8 na walei 17[2]) walikamatwa, walitukanwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597, huku wakifurahia neema ya kuuawa namna ileile ya Yesu.
Hadi sasa Wafiadini wa Japani waliotangazwa watakatifu ni 42, mbali na wenye heri 393.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Kati yao Paulo Miki na Yohane wa Goto walikuwa Wajesuiti; Petro Baptista, Martino wa Kupaa na Fransisko Blanco, walikuwa mapadri wa shirika la Ndugu Wadogo Pekupeku; Filipo wa Yesu, Gonzalo Garcia na Fransisko wa Mt. Mikaeli walikuwa mabradha wa shirika hilohilo; Leo Karasuma, Petro Sukejiro, Kosma Takeya, Paulo Ibaraki, Tomaso Danki, Paulo Suzuki walikuwa makatekista Wajapani; Ludoviko Ibaraki, Antoni wa Nagasaki, Mikaeli Kozaki na mwanae Tomaso, Bonaventura, Gabrieli, Yohane Kinuya, Matia, Fransisko wa Meako, Yohakimu Sakakibara na Fransisko Adaukto walikuwa Wakristo wapya.
Marejeo
hariri- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1282
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |