Funguvisiwa la Lamu

(Elekezwa kutoka Funguvisiwa ya Lamu)

Funguvisiwa la Lamu ni kundi la visiwa katika Bahari Hindi mbele ya pwani ya Kenya kaskazini ambavyo ni sehemu ya Kaunti ya Lamu, Kenya.

Ramani ya funguvisiwa la Lamu: Lamu, Manda, Pate.

Visiwa vikubwa ni Pate, Manda na Lamu. Visiwa vidogo ni pamoja na Kiwayu na Manda Toto.

Mji mkubwa zaidi ni Lamu kwenye Kisiwa cha Lamu. Mji huu uko katika orodha ya Urithi wa dunia ya UNESCO.

Funguvisiwa la Lamu lina sehemu mbalimbali zenye mabaki muhimu ya kiakiolojia kutoka vyanzo vya utamaduni wa Waswahili kama vile Takwa na mji wa Manda halafu Shanga, Pate.

Kuna taarifa ya kwamba jahazi za kundi la meli la Zheng He zilizama karibu na Lamu mnamo mwaka 1415.[1] Mabaharia wa jahazi hizi walibaki kwenye visiwa na kuoa wanawake wa huko. Uchunguzi wa DNA wa wenyeji umethibitisha kuwepo kwa damu ya Kichina.[2] [3][4]

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Engel, Ulf; Ramos, Manuel João (17 May 2013). African Dynamics in a Multipolar World. BRILL. ISBN 978-90-04-25650-7.
  2. Eliot, uk. 11
  3. "Kenyan girl with Chinese blood steals limelight". Chinese Embassy in Kenya. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 8, 2013. Iliwekwa mnamo 3 Aprili 2009. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Kristof, Nicholas D.. "1492: The Prequel", The New York Times, 6 June 1999. Retrieved on 3 April 2009. 

Kujisomea

hariri
  • Allen, James de Vere: Lamu, with an appendix on Archaeological finds from the region of Lamu by H. Neville Chittick. Nairobi: Kenya National Museums.
  • Eliot, Charles (1966). The East African Protectorate. Routledge. ISBN 0-7146-1661-3. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Engel, Ulf; Ramos, Manuel João (17 Mei 2013). African Dynamics in a Multipolar World. BRILL. ISBN 978-90-04-25650-7. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Martin, Chryssee MacCasler Perry; Martin, Esmond Bradley: "Quest for the Past: An Historical Guide to the Lamu Archipelago" Marketing and Publishing Ltd., 1973.

2°06′12″S 41°01′14″E / 2.10333°S 41.02056°E / -2.10333; 41.02056