Gaetano wa Thiene
Gaetano wa Thiene (Vicenza, 1 Oktoba 1480 – Napoli, 7 Agosti 1547), alikuwa padri wa Italia ambaye alichangia sana uamsho wa Kanisa wakati wa Urekebisho wa Kikatoliki hasa kwa njia ya aina mpya ya utawa aliyoianzisha, maarufu kwa jina la Wateatini, aliowaachia jukumu la kufuata mtindo wa maisha ya Mitume wa Yesu. Kwa shirika hilo alifungua njia kwa mashirika mengine kama la Wajesuiti, la Wabarnaba na la Wasomaski.
Huko Napoli alijitosa katika matendo ya huruma, hasa kwa ajili ya waliopatwa na magonjwa wasiotibika, na kuhamasisha vyama kwa ajili ya malezi ya Kikristo ya walei [1].
Alitangazwa na Papa Urban VIII kuwa mwenye heri tarehe 8 Oktoba 1629, halafu Papa Klementi X alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Aprili 1671.
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Catholic Encyclopedia: St Cajetan
- Patron Saints Index: Saint Cajetan Archived 10 Mei 2013 at the Wayback Machine.
- [1]
- Statue of St Cajetan in St Peter's Basilica
- [http://web.archive.org/20061103234403/http://www.sancayetano.org.ar/vidadesc.htm Archived 3 Novemba 2006 at the Wayback Machine. Maisha yake kwa Kihispania]
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |