Galla wa Roma (alifariki Roma, Italia, 546 hivi) alikuwa mwanamke Mkristo wa mmoja kati ya koo bora za mji huo[1].

Baada ya kifo cha mume wake, aliyeishi naye mwaka mmoja, alianzisha monasteri na hospitali karibu na Basilika la Mt. Petro, alipojitosa katika sala na katika huduma kwa wahitaji pamoja na kufunga chakula na kutenda mema mengine.

Sifa zake zinajulikana kupitia kitabu cha Majadiliano cha Papa Gregori Mkuu[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 6 Aprili[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.