Ghuba ya Kalifornia

(Elekezwa kutoka Ghuba ya California)

Ghuba ya California (pia: Bahari ya Cortez, inajulikana kwa lugha ya Kihispania kama Mar de Cortes au Golfo de California. kwa Kiingereza: Gulf of California) ni sehemu ya bahari iliyopo kati ya rasi ya Baja California na Meksiko bara. Eneo lake ni kama km² 160,000.

Eneo la Ghuba ya Kalifornia.
Picha ya Ghuba kutoka satelaiti ya NASA.

Jina na mipaka

hariri

Imepakana na majimbo ya Baja California, Baja California Sur, Sonora, na Sinaloa.

Kwenye ramani za kimataifa huitwa zaidi "Ghuba ya Kalifornia". Watu wa maeneo jirani hupendelea jina "Bahari ya Cortes" kwa kumbukumbu ya Hernando Cortes, mtekaji Mhispania wa Mexiko.

Jiolojia

hariri

Ghuba ya California ilitokea miaka milioni 5.3 iliyopita kutokana na miendo katika ganda la Dunia iliyoitenga na bamba la Amerika ya Kaskazini na kufanywa kama sehemu za uso wa sayari zilipohamisha Hifadhi ya Baja California mbali na Bamba la Amerika Kaskazini.

Volkeno zilitokea katika mchakato huo na kisiwa cha Isla Tortuga ni mfano mmojawapo wa volkano zinazopatikana. [1]

Visiwa

hariri

Ndani ya ghuba kuna visiwa viwili vikubwa, Isla Ángel de la Guarda na Kisiwa cha Tiburon, pamoja na visiwa vingine vidogo.

Marejeo

hariri
  1. "Science Plans RCL". review.nsf-margins.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-18. Iliwekwa mnamo 2008-05-27.

Tovuti za Nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ghuba ya Kalifornia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.