Gorgonia wa Nazienzi

Gorgonia wa Nazienzi (alifariki 23 Februari 375) alikuwa mtoto wa Gregori Mzee na Nona, hivyo dada wa Gregori wa Nazianzo na Sesari wa Nazianzo. Aliishi huko Kapadokia, mkoa wa Dola la Roma katikati ya Uturuki wa leo.

Mt. Gorgonia.

Katika ndoa yake alizaa watoto wengiwengi na kuwaleta wote kwa Kristo pamoja na mume wake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu pamoja na familia yake yote ya asili.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake au tarehe 9 Desemba[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.