Henri Walpole, S.J. (Docking, Norfolk, 24 Januari, 1558York, 7 Aprili 1595) alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uingereza.

Mt. Henri alivyochorwa.

Baada ya kushuhudia kifodini cha Edmundi Campion (1581) alishika imani hadi kupewa upadrisho huko Paris, Ufaransa (1588), alijiunga pia na Wajesuiti.

Alipokuwa tena Uingereza kufanya utume kinyume cha sheria za nchi wakati wa malkia Elisabeti I alikamatwa na kufungwa, aliteswa kikatili na hatimaye alinyongwa na kuraruliwa vipandevipande[1] pamoja na padri mwenzake Aleksanda Rawlins.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929 na mtakatifu na Papa Paulo VI mwaka 1976.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 7 Aprili[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.