Homa ya dengi

(Elekezwa kutoka Homa ya ndengi)

Homa ya dengi (pia: ndengi; kwa Kiingereza: Dengue fever) ni ugonjwa wa kitropiki unaosababishwa na virusi vya dengi (Dengue). Mbu wa kike wa aina ya Aedes, hasa A. aegyptindiye anayesambaza virusi hivyo. Homa ya dengi pia hujulikana kama "homa ya kuvunja mifupa" kwa sababu inaweza kuwafanya watu wawe na maumivu makali hadi wahisi kama mifupa yao inavunjika.

Homa ya dengi
Dengue fever
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10A90.
ICD-9061
DiseasesDB3564
MedlinePlus001374
eMedicinemed/528
MeSHC02.782.417.214

Dalili za ugonjwa huu huanza siku tatu hadi kumi na nne baada ya kuambukizwa. Baadhi ya dalili ni joto jingi mwilini; kuumwa na kichwa; upele unaofanana na na ukambi kwenye ngozi; na maumivu kwenye misuli na jointi. Kwa watu wachache, homa ya dengi inaweza kubadilika na kuwa aina zinazohatarisha maisha. Ya kwanza ni homa ya dengi ya kuvuja damu, ambayo huifanya mishipa ya damu (mishipa inayobeba damu) kuvuja damu, na viwango vya chini vya pleteleti za damu (inayosababisha kuganda kwa damu). Ya pili ni sindromu ya mshtuko ya dengi, inayosababisha shinikizo la chini la damu .

Kuna aina nne tofauti za virusi vya dengi. Mtu anapoambukizwa na mojawapo ya virusi hivi, basi yeye huwa amepata kinga dhidi ya aina hiyo maishani mwake. Hata hivyo, atakuwa amekingwa dhidi ya aina hizo zingine tatu kwa muda mfupi. Ikiwa baadaye atapata mojawapo ya hizi aina tatu za virusi, ana uwezekano mkubwa wa kuwa na matatizo mabaya.

Kwa kawaida matibabu huchukua siku tatu hadi saba. Mgonjwa asipotibiwa virusi huendelea kukomaa na kuwa wakali, homa hii ikishakuwa kali husababisha kupungua kwa pleteleti za damu au ambapo hutokea shinikizo la chini la damu.

Hakuna dawa ya chanjo inayofanya kazi kuwakinga watu dhidi ya virusi vya dengi. Kuna mambo machache yanayoweza kufanywa ili kuwakinga watu dhidi ya homa ya dengi. Watu wanaweza kujikinga wenyewe dhidi ya mbu na kupunguza viwango vya kuumwa. Wanasayansi pia hupendekeza upunguzaji wa makazi ya mbu unaopunguza idadi ya mbu. Mtu anapopata homa ya dengi, kwa kawaida anaweza kupata nafuu kwa kunywa viowevu vya kutosha, mradi ugonjwa ungali katika viwango vya chini au wa kiasi. Ikiwa mtu ana ugonjwa mkali zaidi anaweza kuhitaji kupewa viowevu kwa njia ya mishipa (viowevu vinavyopeanwa kupitia kwenye mshipa, kutumia sindano na tyubu), au kuwekwa damu (kupewa damu kutoka kwa mtu mwingine).

Dengue imekuwa tatizo la kimataifa tangu Vita vikuu vya pili na ni kawaida katika nchi zaidi ya 110, hasa katika bara la Asia, Amerika Kusini na Afrika. Tangu miaka ya 1960, watu wengi wamekuwa wakipata homa ya dengi. Kila mwaka kati ya watu milioni 50 na 528 huambukizwa na takriban watu 10,000 hadi 20,000 hufa kwa ugonjwa huu.

Watu wanatafiti dawa ya chanjo na tiba ya kutibu virusi hivi moja kwa moja. Pia watu hufanya mambo mengi tofauti kwa makusudi ya kujaribu kuwaangamiza mbu.

Maelezo ya kwanza ya homa ya dengi yaliandikwa mwaka wa 1779. Mapema katika karne ya 20, wanasayansi waligundua kuwa ugonjwa huu husababishwa na virusi vya dengi na kuwa huenezwa na mbu.

Ishara na dalili

hariri
 
Picha inayoonyesha dalili za homa ya dengi

Takribani asilimia 80 ya watu ambao wameambukizwa virusi vya dengi hawana dalili au wana dalili ndogo tu (kama joto jingi la kawaida ).[1][2][3] Takriban asilimia 5 ya watu walioambukizwa (au 5 kwa kila watu 100) huwa wagonjwa zaidi. Katika idadi kidogo ya watu hawa, ugonjwa huu huwa wa kuhatarisha maisha.[1][3] Dalili hutokea kati ya siku 3 na 14 baada ya mtu kutangamana na virusi vya dengi. Mara nyingi dalili hutokea baada ya siku 4 hadi 7.[4] Kwa hivyo, ikiwa mtu atarudi kutoka sehemu ambapo dengi inapatikana sana na awe na joto jingi au dalili zingine baada ya zaidi ya siku 14 tangu siku aliporudi, huenda asiwe na homa ya dengi.[5]

Mara nyingi, watoto wanapokuwa na homa ya dengi, dalili zao huwa sawa na zile za homa ya kawaida augastroenteritisi (au homa ya tumbo; kwa mfano, kutapika na kuhara).[6] Hata hivyo watoto wana uwezekano mkubwa wa kuwa na matatizo hatari kutokana na homa ya dengi.[5]

Mfululizo wa dalili anavyoziona mtaalamu wa afya

hariri
 
Clinical course of dengue fever[7]

Dalili kuu za homa ya dengi ni joto jingi linaloanza kighafla; maumivu ya kichwa (kwa kawaida nyuma ya macho); upele; na maumivu kwenye misuli na jointi. Jina la utani la ugonjwa huu ambalo ni "joto jingi la kuvunja mfupa" linaashiria jinsi maumivu haya yanavyoweza kuwa makali.[1][8]HHoma ya dengi hutokea kwa awamu tatu: joto jingi, kali na kupata nafuu.[7]

Katika awamu ya joto jingi, kwa kawaida mtu huwa na joto jingi lililo juu. Joto jingi mara nyingi huwa zaidi ya digrii 40 Selisiasi (digrii 104 Farenhaiti). Pia mtu huyo anaweza kuwa na maumivu katika mwili wote na kuumwa na kichwa. Awamu hii ya joto jingi hudumu kwa muda wa siku 2 hadi 7 .[8][7] Katika awamu hii takribani asilimia 50 hadi 80 ya watu walio na dalili hupata upele.[8][9] Katika siku ya kwanza au ya pili, upele huu unaweza kuonekana kama wekundu kwenye ngozi. Baadaye, (katika siku ya 4 hadi ya 7) upele huu unaweza kuonekana kama ukambi.[9][10] Madoadoa madogo mekundu(petekia) yanaweza kutokea kwenye ngozi. Madoadoa haya hayatoweki ngozi inapofinywa. Madoadoa haya mekundu husababishwa na kapilari zilizochanika. [7] Mtu huyu anaweza pia kutokwa na damu kidogo kwenye membreni za ute za kinywa na pua.[5][8] Joto hili jingi hupungua na baadaye kurudi kwa siku moja au mbili. Hata hivyo mtindo huu hutendekaki tofauti kwa watu tofauti.[10][11]

Kwa watu wengine, ugonjwa huu huingia katika awamu ya ukali baada ya joto hili jingi kuisha. Awamu hii hudumu siku 1 au 2.[7] Katika awamu hii viowevu vinaweza kujikusanya kwenye kifua nafumbatio. Hii hutendeka kwa sababu mishipa midogo ya damu huvuja. Viowevu hujikusanya na kukomakuzunguka Mwilini. Hii ina maana kuwa ogani muhimu zaidi hazipati damu ya kutosha kama kawaida.[7] Kwa sababu hii ogani hizi hazifanyi kazi kikawaida. Pia mtu huyu anaweza kutokwa na damu nyingi(huwa kutoka kwa ufereji wa utumbo.)[5][7]

Chini ya asilimia 5 ya watu walio na homa ya dengi hupata mshtuko kwenye mzunguko wa damu, sindromu ya mshtuko ya dengi, na homa ya dengi ya isababishayo kutoka kwa damu.[5] Iwapo mtu amewahi kuwa na aina nyingine ya dengi hapo awali ("maambukizi ya mara nyingine"), wana uwezekano wa kuwa na matatizo haya mabaya.[5][12]

Katika awamu ya kupata nafuu, viowevu vilivyovuja kutoka kwa mishipa ya damu hurudishwa kwenye damu.[7] Awamu ya kupona hudumu kwa muda wa siku 2 hadi 3.[5] Mara nyingi mtu hupata afueni katika awamu hii. Hata hivyo wanaweza kuwa na muwasho mkali na kiwango cha upigaji wa moyo cha chini.[5][7] Katika awamu hii mtu anaweza kujipata katika hali ambapo viowevu vingi zaidi hurudishwa. Iwapo ugonjwa huu utaathiri ubongo, unaweza kusababisha matukutiko au kiwango cha fahamu kilichogeuka (ambapo kufikiria, kufahamu na tabia za mtu zinazaweza kuwa tofauti na za kawaida).[5]

Matatizo yanayohusiana na homa ya dengi

hariri

Wakati mwingine, ingawa si mara kwa mara, dengi inaweza kuathiri mifumo mingine mwilini.[7] Mtu anaweza kuwa na dalili pekee au pamoja na dalili kuu za dengi.[6] Upungufu katika kiwango cha fahamu hutokea katika asilimia 0.5-6 ya hali kali za ugonjwa huu. Hii inaweza kutendeka virusi vya dengi vinaposababisha maambukizi kwenye ubongo. Pia inaweza kutendeka wakati ambapo ogani muhimu kama ini hazifanyi kazi sawa sawa.[6][11]

Magonjwa mengine ya nurolojia (magonjwa yanayoathiri ubongo na neva) yameripotiwa kwa watu walio na homa ya dengi. Kwa mfano dengi inaweza kusababisha sindromu ya kukingama ya mieliti na ya Guillain-Barré.[6] Ingawa hii huenda isitokee, dengi inaweza kusababisha maambukizi kwa moyo na ini kutofanya kazi.[5][7]

Kisababishi

hariri

Picha itokanayo na uchunguzi wa hadubini ikionyesha virusi vya dengi Homa ya dengi husababishwa na virusi vya dengi. Katika mfumo wa sayansi unaotoa majina na kuainisha virusi, virusi vya dengi viko katika familia ya Flaviviridae na jenasi Flavivirus. Virusi vingine pia viko katika familia hii na husababisha ugonjwa kwa wanadamu. Kwa mfano virusi vya, homa ya majano West Nile virus, virusi vya ensefalitisi vya St. Louis, virusi vya ensefalitisi vya Japanese, kupe-virusi vya mifupa vya ensefalitisi, virusi vya ugonjwa wa Kyasanur forest, na virusi vya Omsk visababishavyo joto jingi mwilini na kuvuja kwa damu vyote ni vya familiaFlaviviridae..[11] Vingi vya virusi hivi huenezwa na mbu au kupe.[11]

Ueneaji

hariri
 
Mbu aina ya Aedes aegypti akila kutoka kwa mwanadamu

Virusi vya dengi mara nyingi huenezwa na mbu, hasa aina yaAedes, .[2] Mbu hawa huishi baina ya latitudo za digrii 35 Kaskazini na 35 Kusini, chin ya kimo cha mita 1000.[2] Mara nyingi wao huuma wakati wa mchana.[13] Kuumwa mara moja tu kunaweza kumuambukiza mtu.[14]

Wakati mwingine mbu pia wanaweza kupata dengi kutoka kwa wanadamu. Mbu wa kike anaweza kuvipata virusi vya dengi akimuuma mtu aliyeambukizwa virusi hivi. Mwanzoni virusi huishi katika seli zilizo kwenye utumbo wa mbu huyo. Takriban siku 8 hadi 10 badaye, virusi hivi huenea kwenye tezi za mate za mbu zinazotengeneza mate. Hii ina maana kuwa mate anayotengeneza mbu huyu yameambukizwa virusi vya homa ya dengi.. Kwa hivyo, mbu anapomuuma mwanadamu, mate yake yaliyoambukizwa huingia mwilini mwa mwanadamu huyo na yanaweza kumuambukiza. Virusi havi havionekani kusababisha matatizo yoyote kwa mbu walioambukizwa, na ambao wataishi na virusi hivi maisha yao yote. Mbu wa aina ya Aedes aegypti ndiye aliye na uwezekano mkubwa wa kueneza dengi. Hii ni kwa sababu yeye hupenda kuishi karibu na wanadamu na kula kutoka kwa watu badala ya wanyama.[15] Pia hupenda kutaga mayai yake kwenye vyombo vya maji vilivyotengwenezwa na watu.

Ugonjwa wa dengi unaweza pia kuenezwa kupitia bidhaa za damu zilizoambukizwa, na utoaji wa ogani.[16][17] Ikiwa mtu aliye na dengi atatoa damu au ogani, ambayo itapewa mtu mwingine, mtu huyo anaweza kupata dengi kutoka kwa damu au ogani aliyopewa. Katika nchi zingine kama Singapore, dengi imeenea sana. Katika nchi hizi, upokeaji damu kati ya 1.6 na 6 kwa kila watu 10,000 hueneza dengi.[18]Virusi vya dengi pia vinaweza kuenezwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto wakati wa ujauzito au mtoto anapozaliwa.[19] Dengi kamwe haienezwi kwa njia nyingine yoyote.[8]

Hatari

hariri

Watoto walio na dengi wana uwezekano mkubwa wa kuwa wagonjwa sana kuliko watu wazima. Watoto wana uwezekano mkubwa wakuwa wagonjwa sana iwapo wana afya na wamelishwa vizuri.[5] (Hii ni tofauti na maambukizi mengine mengi ambayo kwa kawaida huwa mabaya zaidi kwa watoto walio na utapiamlo, hawana afya au hawajalishwa vizuri.) Wanawake wana uwezekano mkubwa wa kuwa wagonjwa sana kuliko wanaume.[20] Dengi inaweza kuwa ya kuhatarisha maisha kwa watu walio na magonjwa yanayodumu kwa muda mrefu kama kisukari na pumu.[20]

Utaratibu

hariri

Mbu anapomuuma mtu, mate yake huingia katika ngozi ya mtu huyu. Virusi hubebwa kwenye mate ya mbu huyu iwapo ana dengi. Kwa hivyo, mbu anapomuuma mtu, virusi huingia kwenye ngozi yake pamoja na mate ya mbu. Virusi hujishikiza na kuingia katika seli nyeupe za damu yake. (Seli nyeupe za damu zinafaa kuukinga mwili kwa kupigana na hatari kama maambukizi.) Seli nyeupe za damu zinapozunguka mwilini, virusi hivi huzaana. Seli nyeupe za damu hujibu kwa kutoa ishara nyingi protini (ziitwazo saitokini), kama vile intalukini, intaferoni na tumonekrosisi. Protini hizi husababisha joto jingi, dalili kama za homa na maumivu makali ambayo ni sifa bainifu ya dengi.

Ikiwa mtu ana maambukizi makali, virusi huzaana kwa haraka zaidi mwilini. Kwa kuwa kuna virusi vingi zaidi, vinaweza kuathiri ogani zingine nyingi (kama vile ini nauboho wa mfupa). Viowevu kutoka kwenye damu huvuja kupitia kuta za mishipa midogo ya damu na kuingia kwenye kaviti za mwili. Kwa sababu hii, ni kidogo cha damu inayozunguka mwilini kwenye mishipa ya damu. Shinikizo la damu ya mtu huyu huwa chini sana kiasi kwamba moyo hauwezi kusambaza damu ya kutosha kwa ogani muhimu. Pia uboho wa mfupa hauwezi kutengeneza pleteleti za kutosha zinazohitajika kwa ugandaji bora wa damu. Bila pleteleti za kutosha, mtu huyu ana uwezekano mkubwa wa kuwa na matatizo ya kuvuja damu. Kuvuja damu ni tatizo kubwa la dengi (mojawapo ya matatizo makali yanayoweza kusababishwa na ugonjwa huu).[21]

Utambuzi

hariri

Kwa kawaida wataalamu wa huduma za afya hutambua dengi kwa kumchunguza mtu aliyeambukizwa na kugundua kuwa dalili zake zinalingana na dengi. Wataalamu wa huduma za afya wana uwezo hasa wa kuweza kutambua dengi kwa njia hii katika sehemu ambapo dengi imeenea sana.[1] Hata hivyo, dengi inapokuwa katika awamu za mwanzo, inaweza kuwa vigumu kuitofautisha na maambukizi mengine ya virusi.[5] Mtu anaweza kuwa na dengi iwapo ana joto jingi na mbili za dalili hizi : kichefuchefu na kutapika; upele; maumivu kwa mwili wote; idadi ya chini ya seli nyeupe za damu ; au virusi kutambuliwa kupitia kipimo cha damu cha toniketi. Dalili yoyote ya hatari, pamoja na joto jingi huwa ishara kuwa mtu ana dengi katika sehemu ambapo dengi imeenea sana[22].

Dalili za hatari hujitokeza kabla ya dengi kuwa kali.[7] Kipimo cha toniketi ni muhimu wakati ambapo kipimo cha maabara hakiwezi kufanyika. Ili kufanya kipimo cha tomiketi, mtaalum wa huduma za afya atafunga sijafu ya shinikizo la damu kwenye mkono wa mtu kwa muda wa dakika 5. Kisha mtaalum huyo wa huduma za afya atahesabu madoadoa yoyote mekundu kwenye ngozi. Idadi kubwa ya madoadoa humaanisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mtu huyu kuwa na homa ya dengi.[7] Inaweza kuwa vigumu kueleza tofauti kati ya homa ya dengi na chikungunya. Chikungunya ni mojawapo yamaambukizi ya virusi ulio na dalili sawa na homa ya dengi, na aidha hutokea katika sehemu sawa duniani.[8] Homa ya dengi inaweza pia kuwa na dalili sawa na zile za magonjwa mengine kamamalaria, leptospirosisi, homa ya matumbo, na ugonjwa wa uvimbe wa tando za uti wa mgongo na ubongo wa watoto. Mara nyingi, kabla ya mtu kutambuliwa kuwa na ugonjwa wa dengi, mhudumu wake wa afya atampima kuhakikisha hana mojawapo ya magonjwa haya.[5]

Mtu anapokuwa na homa ya dengi, badiliko la kwanza linaloweza kuonekana kwenye vipimo vya maabara ni upungufu wa seli nyeupe za damu. Idadi ndogo ya pleteleti na ongezeko la asidi ya umetaboli pia ni dalili za homa ya dengi.[5] Ikiwa mtu huyu ana homa kali sana ya dengi i kuna mabadiliko mengine yanayoweza kuonekana kwenye damu yake ikichunguzwa. Homa kali ya dengi inaweza pia kusababisha viowevu kuvuja kutoka kwenye mfumo wa damu. Hii husababisha ukolezi wa damu (ambapo kuna plazma kidogo - sehemu ya majimaji ya damu - na seli nyekundu za damu zaidi kwenye damu). Pia husababisha viwango vya chini vya alibumini kwenye damu[5]

Wakati mwingine, homa kali ya dengi husababisha efusheni (ambapo kiowevu kilichomiminika hukusanyika kwenyemapafu au asitisi (ambapo kiowevu hukusanyika kwenye fumbatio). Ikiwa mikusanyiko hii ni mikubwa vya kutosha, mtaalam wa afya anaweza kuitambua anapomchunguza mtu huyu vipimo[5] Mtaalam wa afya anaweza kutambua sindromu ya mshtuko ya dengi mapema ikiwa ataweza kutumial Altrasaundi ili kupata kiowevu ndani ya mwili.[1][5] Hata hivyo, katika maeneo mengi ambapo homa ya dengi imeenea sana, wahudumu wengi wa afya na kliniki hawana mashine ya altrasaundi.[1]

Uainishaji

hariri

Katika mwaka wa 2009Shirika la Afya Duniani (WHO) liliainisha au liligawa homa ya dengi katika aina mbili: isiyo na utata, na kali.[1][22] Kabla ya haya, mnamo mwaka wa 1997, shirika la afya duniani liligawanya ugonjwa huu katika homa isiyotofautishwa, homa ya dengi na homa ya kihemorajiki ya dengi. Shirika la afya duniani lilifanya uamuzi kuwa njia hii ya kugawanya homa ya dengi na ambayo ni ya zamani ilistahili kufanywa kwa njia rahisi. Pia liliamua kuwa njia hiyo ya zamani ilikuwa zuivu: haikuonyesha njia zote ambamo homa ya dengi inaweza kujitokeza. Ingawa uainishaji wa homa ya dengi ulibadilishwa kirasmi, uainishaji wa kale bado unatumika mara kwa mara.[22][5][23]

Katika mfumo wa kale wa shirika la afya duniani wa uainishaji, homa ya kihemorajiki ya dengi iligawanywa katika viwango vinne vinavyoitwa awamu ya I–IV:

  • Katika awamu ya I, mtu huyo ana joto jingi mwilini. Anavilia kwa urahisi au virusi hupatikana baada ya vipimo vya damu kwa kutumia toniketi.
  • Katika awamu ya II, hutokwa na damu katika ngozi na sehemu zingine za mwili.
  • Katika awamu ya III, mtu huyo huonyesha daliliza mshtuko kwenye mzunguko wa damu.
  • Katika awamu ya IV mtu huyo ana mshtuko mkali kiasi kwamba shinikizo la damu pamoja na mpigo wa moyo haviwezi kusikika[23]Awamu za III na IV huitwa"sindromu ya mshtuko ya homa ya dengi."[22][23]

Vipimo vya maabara

hariri

Homa ya dengi inaweza kutambuliwa kwa vipimo vya maabara vya mikrobiolojia .[22]Vipimo vingine vichache tofauti vinaweza kufanywa. Kipimo kimoja (utengaji wa virusi) hutenga (au kugawanya) virusi vya homa ya dengi kwenye vikuza viini (au sampuli) za seli. Aina nyingine ya kipimo (utambuzi wa asidi za kiiniseli) hutafuta asidi za kiiniseli kwenye virusi kwa kutumia ufundi sanifu uitwao msururu wa athari za polima (PCR). Kipimo cha tatu (utambuzi wa antijeni) hutafuta antijeni kwenye virusi. Kipimo hutafuta kwenye damu antibodi zinazotengenezwa na mwili ili kupigana na virusi vya homa ya dengi[20][24] Vipimo vya utengaji wa virusi na utambuzi wa asidi za kiiniseli ni bora kuliko utambuzi wa antijeni. Hata hivyo, gharama ya vipimo hivi ni ghali Na kwa hivyo havipatikani katika sehemu nyingi.[24] Homa ya dengi inapokuwa katika awamu za kwanza , vipimo vinaweza kuwa hasi (kumaanisha havionyeshi kuwa mtu huyo ana ugonjwa huo).[5][20]

Isipokuwa vipimo vya antibodi, vipimo hivi vya maabara vinaweza kusaidia kutambua homa ya dengi katika awamu ya (mwanzoni) kwanza ya ugonjwa pekee. Hata hivyo, vipimo vya antibodi vinaweza kudhibitisha kuwa mtu ana homa ya dengi katika awamu za mwisho za maambukizi. Mwili hutengeza antibodi maalum ambazo hupigana na virusi vya homa ya dengi baada ya siku 5 hadi 7[8][20][25]

Hakuna chanjo zilizoidhinishwa kuwakinga watu kutokana na virusi vya homa ya dengi.[1] Ili kuzuia maambukizi, Shirika la afya duniani lilipendekeza kudhibiti idadi ya mbu na kuwakinga watu dhidi ya kuumwa na mbu.[13][26]

Shirika la afya duniani lilipendekeza mpango wa kuzuia homa ya dengi (unaoitwa mpango "unganifu wa kudhibiti vekta") ulio na sehemu tano tofauti:

  • Utetezi, uhamasisho wa jamii, na Utungaji sheria (sheria) unafaa kutumiwa kuimarisha mashirika ya afya ya umma na jamii
  • Sehemu zote za jamii zinafaa kufanya kazi pamoja. Hii ni pamoja na Sekta ya umma (kama vile serikali), sekta ya kibinafsi (kama vile biashara na mashirika), na sekta ya huduma ya afya
  • Njia zote za kudhibiti magonjwa zinafaa kuunganishwa (au kuletwa pamoja), ilirasilimali zilizoko ziweze kuwa na athari kubwa.
  • Uamuzi unafaa kufanywa kulingana na ushahidi. Hii itahakikisha kuwa tatuzi (vitu vinavyofanywa ili kuzuia homa ya dengi) zina manufaa.
  • Maeneo ambapo homa ya dengi ni tatizo yanafaa kupata usaidizi ili yaweze kuongeza uwezo wao wa kukabiliana na ugonjwa huu wenyewe.[13]

Shirika la afya duniani pia linapendekeza kufanya vitu maalum ili kudhibiti mbu na kuwakinga watu dhidi ya kuumwa. Njia bora zaidi ya kudhibiti aina ya " Aedes aegypti" ni kuharibu makazi yake.[13] Watu wanafaa kumwaga maji yaliyo kwenye vyombo katika mazingira yao ( ili mbu wasitage mayai humo ndani). Viua wadudu au mbinu zaki kibayolojia vinaweza pia kutumika katika kudhibiti mbu katika maeneo haya.[13] Wanasayansi wanafikiri kuwa kunyunyiza otganofosfati au kiua wadudu cha pairethroidi hakusaidii.[3] Maji yaliyosimama (yasiyotiririka) yanafaa kutolewa kwasababu yanavutia mbu na pia watu wanaweza kuwa na matatizo ya kiafya ikiwa viua wadudu vitaongezeka kwa maji yaliyosimama[13] Ili kuzuia kuumwa na mbu, watu wanaweza kuvaa nguo zinazofunika ngozi yao kikamilifu. Wanaweza kutumia vizuia wadudu (kama vile viowevu vya kuua wadudu), ambayvo husaidia kuwafukuza mbu. (DEET ni bora zaidi) Watu wanaweza pia kutumia neti wanapopumzika.[14]

Udhibiti

hariri

Hakuna tiba maalum ya homa ya dengi.[1] Watu tofauti wanahitaji matibabu tofauti kulingana na dalili zao. Watu wengine hupata nafuu kwa kunywa vinywaji tu nyumbani wahudumu wao wa afya wakifuatilia ili kuhakikisha wanapata nafuu. Watu wengine wanahitaji dawa za kupitishwa kwenye mishipa na kupewa damu.[27]Mtaalam wa afya anaweza kuamua kumlaza hospitalini ikiwa ana dalili mbaya za hatari, hasa ikiwa ana hali mbaya ya kiafya inayodumu kwa muda mrefu.[5]

Watu walioambukizwa wanapohitaji viowevu kupitia kwenye mshipa, kwa kawaida huvihitaji kwa siku moja au mbili.[27] Mtaalam wa afya ataongeza kiwango cha viowevu anavyopewa ili mtu huyo aweze kutoa kiwango fulani cha mkojo (0.5–1 mL/kg/hr). Kiowevu hicho huongezwa hadi hematokriti ya mtu huyo (kiwango cha ayoni kwenye damu) na ishara muhimu kurejea katika hali yake ya kawaida.[5] Kwa sababu ya hatari ya kutokwa na damu, wataalam wa huduma za afya hujaribu kujitenga nataratibu za kiafya zenye madhara kama vile intubesheni ya nasogastri (kuweka tyubu kwenye pua la mtu na kuiteremsha hadi kwenye tumbo), kudunga sindano kwenye misuli (kumpa mtu dawa kwenye misuli moja kwa moja) na kwenye mianya ya ateri (kuweka sindano kwenye ateri).[5] Asetaminofeni (Tylenol) inaweza kutumiwa kudhibiti homa na maumivu. Aina ya dawa ya kuzuia kuvimba inayoitwa NSAID (kama vile ibuprofeni na asprini) hazifai kutumiwa kwa sababu zinaweza kusababisha kutokwa na damu.[27] Kupewa damu kunafaa kuaza mapema iwapo ishara kuu za mtu huyu zitabadilika au si za kawaida na ikiwa idadi ya seli nyekundu za damu inapungua.[28] Ikiwa damu itahitajika, mtu anafaa kupata damu nzima (damu ambayo haijagawanywa katika sehemu tofauti) au kundi la seli nyekundu za damu. Pleteleti (zilitengwa kutoka kwa damu nzima) na plazma – mbichi iliyoganda huwa haipendekezwi.[28]

Mtu anapokuwa katika awamu ya kupata nafuu kutokana na homa ya dengi, hatapewa tena viowevu kupitia mishipani ili asiweze kupata limbiko la viowevu mwilini mwake.[5] Ikiwa kiowevu kitakuwa kingi na dalili kuu ziwe dhabiti(zisizobadilika) ni vyema kuacha kumpa viowevu zaidi.[28] Ikiwa mtu hako tena katika awamu ya hatari ya ugonjwa huu, anaweza kupewa diuretiki ya kitanzi kama vile furosemidi (Lasix). Hii inaweza kusaidia kuondoa viowevu zaidi kwenye damu yake.[28]

Uwezekano

hariri

Watu wengi walio na homa ya dengi hupata nafuu na hawapati matatizo yoyote baadaye.[22] Bila matibabu, asilimia 1 hadi 5 ya watu walioambukizwa (1 hadi 5 katika kila watu 100) hufariki kutokana na homa ya dengi.[5] Kwa kupata matibabu yanayofaa, chini ya asilimia 1 hufariki.[22] Hata hivyo, kwa watu walio na homa kali ya dengi, asilimia 26 hufariki (26 kwa kila 100)[5]

Homa ya dengi imeenea sana katika zaidi ya nchi 110.[5] Kila mwaka, watu milioni 50 hadi 100 ulimwenguni huambukizwa. Pia husababisha watu nusu milioni kulazwa hospitalini[1] na takriban vifo 12,500 hadi 25,000 ulimwenguni kila mwaka.[6][29]

Homa ya dengi ndio ugonjwa wa virusi ulioenea sana ambao huenezwa na wadudu.[12] Homa ya dengi inakisiwa kuweza kusababisha ulemavu kwa maisha ya mtu kwa taktiban miaka 1600 kwa kila milioni moja ya watu. Hii ina maana kuwa kwa kila milioni moja ya watu, homa ya dengi husababisha takriban miaka 1600 ya maisha kupotea. Hii ni takriban ni karibu sawa na athari zinazosababishwa na magonjwa mengine ya utotoni na ya tropiki kama vile kifua kikuu.[20] Homa ya dengi inakisiwa kuwa ugonjwa wa pili muhimu wa tropiki baada yamalaria.[5] Shirika la afya duniani pia huainisha denge kama mojawapo wa magonjwa 16 ya tropiki yaliyotelekezwa (kumaanisha kuwa haichukuliwi kuwa jambo zito ipasavyo).[30]

Homa ya dengi inazidi kuenea ulimwenguni. Katika mwaka wa 2010, homa ya dengi ilikuwa imeenea mara 30 zaidi ikilinganishwa na mwaka wa 1960.[31] Mambo mengi yanakisiwa kusababisha kuongezeka kwa denge. Watu wengi wanaishi mijini. Idadi ya watu ulimwenguni inaongezeka. Watu wengi wanasafiri kimataifa ( kati ya nchi). Halijoto duniani pia inakisiwa kusababisha ongezeko la homa ya dengi.[1]

Homa ya dengi hutokea sana katika eneo laikweta. Watu bilioni 2.5 wanaishi katika maeneo ambapo homa ya dengi hutokea. Asilimia 70 ya watu hawa wanaishi Asia na Pasifiki.[31] Marekani asilimia 2.9 hadi 8 ya watu wanaorudi kutoka katika sehemu zilizo na homa ya dengi na wana joto jingi, waliambukizwa walipokuwa wakisafiri[14] Katika kundi hili la watu, homa ya dengi ndiyo maambukizi ya pili katika kuenea yaliyotambuliwa baada ya malaria[8]

Historia

hariri

Mara ya kwanza kuandika kuhusu dengi ilikuwa takribani miaka mingi iliyopita. Ensaiklopidia ya tiba ya Uchina kutoka katika Nasaba ya Jin (iliyokuwepo tangu 265 hadi 420 AD) ilizungumzia kumhusu mtu ambaye huenda alikuwa na homa yadengi. Kitabu hicho kilizungumzia "sumu ya maji" iliyosababishwa na wadudu wanaopaa.[32][33]Kunazo pia nakala zilizoandikwa tangu karne ya 17 (miaka ya 1600) kuhusu kinachoweza kuwa epidemiki ya homa ya dengi (ambapo ugonjwa huo ulienea kwa haraka kwa muda mfupi). Ripoti za hapo awali za epidemiki ya homa ya dengi huenda ni za tangu mwaka ya 1779 na 1780. Ripoti hizi zinazungumzia epidemiki iliyomaliza Asia, Afrika na Kaskazini mwa Marekani.[33] Tangu wakati huo hadi mwaka wa 1940, hapakuwa na epidemiki nyingine nyingi.[33]

Katika mwaka wa 1906, wanasayansi walidhibitisha kuwa watu walipata maambukizi kutokambu aina ya Aedes. Katika mwaka wa 1907, wanasayansi walionyesha kuwa homa ya dengi husababishwa na virusi. Huu ulikuwa ugonjwa wa pili kuonyeshwa kusababishwa na virusi. (Wanasayansi walikuwa tayari washadhibitisha kuwa virusi husababisha homa ya manjano).[34]John Burton Cleland na Joseph Franklin Siler walizidi kutafiti kuhusu virusi vya homa ya dengi,na kutambua jinsi vinavyoenea.[34]

Homa ya dengi ilianza kuenea kwa haraka katika na baada ya Vita vya Pili Duniani. Hii inakisiwa kuwa kutokana na vita kubadili mazingira kwa njia tofauti. Aina tofauti za homa ya dengi pia huenea katika maeneo mapya. Kwa mara ya kwanza watu walianza kupata homa ya kihemorajiki ya dengi. Aina hii kali ya ugonjwa huu iliripotiwa kwa mara ya kwanza nchini Ufilipino mnamo mwaka wa 1953. Kufikia miaka ya 1970, homa ya kihemorajiki ya dengi ilikuwa kisababishi kikuu cha vifo kwa watoto. Ilikuwa pia imeanza kutokea Marekani na Pasifiki.[33] Homa ya kihemorajiki ya dengi na dalili za sindromu ya mshtuko ya dengi ziliripotiwa kwa mara ya kwanza katika Marekani ya Kati na Kusini mwaka wa 1981. Wakati huu, wataalam wa afya waligundua kuwa watu ambao walikuwa tayari wamepata aina ya 1 ya virusi vya dengi walikuwa wakipata aina ya 2 miaka michache baadaye.[11]

Historia ya neno hili

hariri

Haijulikani sana mahali ambapo neno "dengi" lilitokea. Watu wengine hukisia kuwa linatoka katika Swahili kirai Ka-dinga pepo Kirai hiki kinazungumzia kuhusu huo ugonjwa kusababishwa na pepo za kishetani[32] Neno la kiswahili dinga linakisiwa kutoka katika neno la Kihispania dengi. Neno hili linamaanisha "makini". Huenda neno hilo lilitumika kumwelezea mtu aliyeathiriwa na maumivu ya mifupa yanayotokana na homa ya dengi; uchungu huo ungemfanya mtu kutembea kwa makini.[35] Hata hivyo, pia kuna uwezekano kuwa neno hilo la Kihispania lilitokea katika lugha ya kiswahili na sio ilivyosemwa hapo awali.[32]

Watu wengine hukisia kuwa neno "dengi" lilitokea nchini West Indies. Nchini West Indies, watumwa walioathiriwa na homa ya dengi walisemekana kusimama na kutembea kama "mlimbwende". Kwa sababu ya haya ugonjwa huo pia uliitwa "homa ya mlimbwende"[36][37]

Neno" homa ya kuvunja mifupa" lilitumika kwa mara ya kwanza na Benjamin Rush aliyekuwa daktari (fizishiani) na "Mwanzilishi". Katika mwaka wa 1789, Rush alitumia jina "homa ya kuvunja mifupa” katika ripoti inayohusu kuzuka kwa dengi mwaka wa 1780 nchini Philadelphia. Katika ripoti hiyo, Rush alitumia sana neno rasmi "homa ya kuondoa nyongo".[38][39] Neno "homa ya dengi halikutumika sana hadi baada ya mwaka wa 1828.[37] Kabla ya hapo, watu tofauti walitumia majina tofauti kwa ugonjwa huo. Kwa mfano, homa ya dengi pia iliitwa "homa ya kuvunja moyo" na "la dengue"[37] Majina mengine pia yalitumika kwa dengi kali: kwa mfano, "thrombocytopenic purpura ya kuambukiza", "Philippine," "Thai," na "homa ya kihemorajiki ya Singapore".[37]

Utafiti

hariri

Wanasayansi wanazidi kufanya utafiti wa njia za kukinga na kutibu homa ya dengi. Watu pia wanajaribu kudhibiti mbu,[40] kutengeneza dawa ya chanjo na kutengeneza dawa ya kupigana na virusi hivi.[26]

Vitu vingi rahisi vimefanywa ili kudhibiti mbu. Vingine vya vitu hivi vimefaulu. Kwa mfano,guppies (Poecilia reticulata) au kopepodi wanaweza kuwekwa kwenye maji yosiyotiririka ili waweze kula Viluwiluwi (mayai) wa mbu.[40]

Wanasayansi wanazidi kujitahidi kutengeneza dawa ya chanjo ya kuwakinga watu kutokana na aina zote nne za dengi.[26] Wanasayansi wengine wanahofia kuwa chanjo inaweza kuongeza hatari zaidi ya ugonjwa huu kupitia uwezekano unaotokana na antibodi “(ADE)”.[41]Chanjo bora zaidi na inayowezekana inaweza kuwa na sifa chache tofauti. Kwanza, itakuwa salama. Pili, itafanya kazi baada ya sindano mbili au tatu. Tatu, itakinga dhidi ya aina zote tatu za virusi vya dengi. Nne, haitasababisha ADE. Tano, itakuwa rahisi kusafirisha na kuweka (kuweka hadi itakapotakikana). Sita, itakuwa ya gharama ya chini na kuwa ya kumudu (bei inayofaa)[41] Chanjo chache zilikuwa zimejaribiwa kufikia mwaka wa 2009.[20][38][41] Wanasayansi wanaamini kuwa dawa ya kwanza ya chanjo itaweza kupatikana madukani ifikiapo mwaka wa 2015.[26]fi

Wanasayansi pia wanazidi kujitahidi kutengeneza dawa za kupigana dhidi ya virusi kutibu maambukizzi ya homa ya dengi na kuwakinga watu kutokana na maabukizi zaidi.[42][43]Pia wanafanya juhudi ili kugundua muundo wa proteni za virusi hivi. Hii inaweza kuwasaidia kutengeneza dawa bora zaidi za kukabiliana na dengi.[43]

Tanbihi

hariri
  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 Whitehorn J, Farrar J (2010). "Dengue". Br. Med. Bull. 95: 161–73. doi:10.1093/bmb/ldq019. PMID 20616106.
  2. 2.0 2.1 2.2 WHO (2009), pp. 14–16.
  3. 3.0 3.1 3.2 Reiter P (2010-03-11). "Yellow fever and dengue: a threat to Europe?". Euro Surveil. 15 (10): 19509. PMID 20403310.
  4. Gubler (2010), p. 379.
  5. 5.00 5.01 5.02 5.03 5.04 5.05 5.06 5.07 5.08 5.09 5.10 5.11 5.12 5.13 5.14 5.15 5.16 5.17 5.18 5.19 5.20 5.21 5.22 5.23 5.24 5.25 5.26 Ranjit S, Kissoon N (2010). "Homa ya kihemorajiki ya dengi na dalili za ugonjwa". Pediatr. Crit Care Med. 12 (1): 90–100. doi:10.1097/PCC.0b013e3181e911a7. PMID 20639791. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 Varatharaj A (2010). "Encephalitis in the clinical spectrum of dengue infection". Neurol. India. 58 (4): 585–91. doi:10.4103/0028-3886.68655. PMID 20739797.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  7. 7.00 7.01 7.02 7.03 7.04 7.05 7.06 7.07 7.08 7.09 7.10 7.11 7.12 WHO (2009) p. 25–27 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "WHOp25" defined multiple times with different content
  8. 8.0 8.1 8.2 8.3 8.4 8.5 8.6 8.7 Chen LH, Wilson ME (2010). "Dengue and chikungunya infections in travelers". Curr. Opin. Infect. Dis. 23 (5): 438–44. doi:10.1097/QCO.0b013e32833c1d16. PMID 20581669. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  9. 9.0 9.1 Wolff K, Johnson RA (eds.) (2009). "Viral Infections of Skin and Mucosa". Fitzpatrick's Color Atlas and Synopsis of Clinical Dermatology (tol. la 6th). New York: McGraw-Hill Medical. ku. 810–2. ISBN 9780071599757. {{cite book}}: |author= has generic name (help)
  10. 10.0 10.1 Knoop KJ, Stack LB, Storrow A, Thurman RJ (eds.) (2010). "Tropical Medicine". Atlas of Emergency Medicine (tol. la 3rd). New York: McGraw-Hill Professional. ku. 658–9. ISBN 0071496181. {{cite book}}: |author= has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  11. 11.0 11.1 11.2 11.3 11.4 Gould EA, Solomon T (2008). "Pathogenic flaviviruses". The Lancet. 371 (9611): 500–9. doi:10.1016/S0140-6736(08)60238-X. PMID 18262042. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  12. 12.0 12.1 Rodenhuis-Zybert IA, Wilschut J, Smit JM (2010). "Dengue virus life cycle: viral and host factors modulating infectivity". Cell. Mol. Life Sci. 67 (16): 2773–86. doi:10.1007/s00018-010-0357-z. PMID 20372965. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  13. 13.0 13.1 13.2 13.3 13.4 13.5 WHO (2009), pp. 59–60.
  14. 14.0 14.1 14.2 Center for Disease Control and Prevention. "Chapter 5 – Dengue Fever (DF) and Dengue Hemorrhagic Fever (DHF)". 2010 Yellow Book. Iliwekwa mnamo 2010-12-23.
  15. Gubler (2010), pp. 377–78.
  16. Wilder-Smith A, Chen LH, Massad E, Wilson ME (2009). "Threat of Dengue to Blood Safety in Dengue-Endemic Countries". Emerg. Infect. Dis. 15 (1): 8–11. doi:10.3201/eid1501.071097. PMC 2660677. PMID 19116042. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  17. Stramer SL, Hollinger FB, Katz LM; na wenz. (2009). "Emerging infectious disease agents and their potential threat to transfusion safety". Transfusion. 49 Suppl 2: 1S–29S. doi:10.1111/j.1537-2995.2009.02279.x. PMID 19686562. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  18. Teo D, Ng LC, Lam S (2009). "Is dengue a threat to the blood supply?". Transfus Med. 19 (2): 66–77. doi:10.1111/j.1365-3148.2009.00916.x. PMC 2713854. PMID 19392949. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  19. Wiwanitkit V (2010). "Unusual mode of transmission of dengue". Journal of Infection in Developing Countries. 4 (1): 51–4. PMID 20130380. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  20. 20.0 20.1 20.2 20.3 20.4 20.5 20.6 Guzman MG, Halstead SB, Artsob H; na wenz. (2010). "Dengue: a continuing global threat". Nat. Rev. Microbiol. 8 (12 Suppl): S7–S16. doi:10.1038/nrmicro2460. PMID 21079655. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  21. Martina BE, Koraka P, Osterhaus AD (2009). "Dengue Virus Pathogenesis: an Integrated View". Clin. Microbiol. Rev. 22 (4): 564–81. doi:10.1128/CMR.00035-09. PMC 2772360. PMID 19822889. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-18. Iliwekwa mnamo 2013-11-28. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  22. 22.0 22.1 22.2 22.3 22.4 22.5 22.6 WHO (2009), pp. 10–11.
  23. 23.0 23.1 23.2 WHO (1997). "Chapter 2: clinical diagnosis". Homa ya kihemorajiki ya homa ya dengi: utambuzi, matibabu, kinga na udhibiti (PDF) (tol. la 2nd). Geneva: World Health Organization. ku. 12–23. ISBN 9241545003.
  24. 24.0 24.1 WHO (2009), pp. 90–95.
  25. Gubler (2010), p. 380.
  26. 26.0 26.1 26.2 26.3 WHO (2009), p. 137. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "WHOp137" defined multiple times with different content
  27. 27.0 27.1 27.2 WHO (2009), pp. 32–37.
  28. 28.0 28.1 28.2 28.3 WHO (2009), pp. 40–43.
  29. WHO media centre (Machi 2009). "Dengue and dengue haemorrhagic fever". World Health Organization. Iliwekwa mnamo 2010-12-27.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  30. WHO media centre. "Diseases covered by NTD Department". World Health Organization. Iliwekwa mnamo 2010-12-27.
  31. 31.0 31.1 WHO (2009), p. 3.
  32. 32.0 32.1 32.2 Anonymous (2006). "Etymologia: dengue" (PDF). Emerg. Infec. Dis. 12 (6): 893.
  33. 33.0 33.1 33.2 33.3 Gubler DJ (1998). "Dengue and Dengue Hemorrhagic Fever". Clin. Vidubini. Rev. 11 (3): 480–96. PMC 88892. PMID 9665979. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-25. Iliwekwa mnamo 2013-11-28. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |month= ignored (help)
  34. 34.0 34.1 Henchal EA, Putnak JR (1990). "The dengue viruses". Clin. Vidubini. Rev. 3 (4): 376–96. doi:10.1128/CMR.3.4.376. PMC 358169. PMID 2224837. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-25. Iliwekwa mnamo 2013-11-28. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |month= ignored (help)
  35. Harper D (2001). "Etymology: dengue". Online Etymology Dictionary. Iliwekwa mnamo 2008-10-05.
  36. Anonymous (1998-06-15). "Definition of Dandy fever". MedicineNet.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-05. Iliwekwa mnamo 2010-12-25.
  37. 37.0 37.1 37.2 37.3 Halstead SB (2008). Dengue (Tropical Medicine: Science and Practice). River Edge, N.J: Imperial College Press. ku. 1–10. ISBN 1-84816-228-6.
  38. 38.0 38.1 Barrett AD, Stanberry LR (2009). Vaccines for biodefense and emerging and neglected diseases. San Diego: Academic. ku. 287–323. ISBN 0-12-369408-6.
  39. Rush AB (1789). "An account of the bilious remitting fever, as it appeared in Philadelphia in the summer and autumn of the year 1780". Medical enquiries and observations. Philadelphia: Prichard and Hall. ku. 104–117.
  40. 40.0 40.1 WHO (2009), p. 71.
  41. 41.0 41.1 41.2 Webster DP, Farrar J, Rowland-Jones S (2009). "Progress towards a dengue vaccine". Lancet Infect Dis. 9 (11): 678–87. doi:10.1016/S1473-3099(09)70254-3. PMID 19850226. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  42. Sampath A, Padmanabhan R (2009). "Molecular targets for flavivirus drug discovery". Antiviral Res. 81 (1): 6–15. doi:10.1016/j.antiviral.2008.08.004. PMC 2647018. PMID 18796313. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  43. 43.0 43.1 Noble CG, Chen YL, Dong H; na wenz. (2010). "Strategies for development of Dengue virus inhibitors". Antiviral Res. 85 (3): 450–62. doi:10.1016/j.antiviral.2009.12.011. PMID 20060421. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)

Marejeo

hariri