Picha takatifu
Picha takatifu (pia "ikona" kutoka Kigiriki εἰκών, eikōn "picha" kwa kupitia Kiingereza icon) kwa kawaida ni mchoro unaoheshimiwa kidini hasa katika Ukristo wa Mashariki lakini pia katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo wa Magharibi, kama vile Kanisa la Kilatini.
Mara nyingi picha hizo zinamhusu Yesu, Bikira Maria, watakatifu wengine, malaika na msalaba.
"Sanaa ya Kikristo" inatajwa kwanza kati ya karne ya 2 na karne ya 3 katika maandishi ya Tertuliani (160 hivi - 220) na Klemens wa Aleksandria (150 hivi - 212).
Matumizi ya picha hizo yalipingwa na baadhi ya Wakristo, hasa wa mashariki, baada ya Uislamu kutokea na kuenea katika maeneo yao. Hapo kaisari Leo III wa dola la Roma Mashariki alikataza picha hizo ili kujilinganisha na Waislamu na kujenga uhusiano mzuri nao.
Kumbe wamonaki na Wakristo wengine wengi walipinga katazo hilo. Ndio mwanzo wa mabishano makubwa yasiyoishia katika hoja na maandishi, bali yalichukua uhai wa watu, hasa waliodhulumiwa na serikali.
Hatimaye Mtaguso wa pili wa Nisea (787) ulithibitisha uhalali wa picha hizo na wa heshima ambazo zinapewa, kama ulivyotetewa hasa na mtakatifu Mwarabu Yohane wa Damasko.
Pamoja na kwamba picha takatifu zinasema na mioyo ya waamini wanyofu, mara nyingi utaalamu wa ikonografia unahitajika hasa katika kufafanua picha takatifu za Ukristo wa Mashariki, kwa kuwa hizo hazilengi kuiga sura halisi zinavyoonekana na macho, bali kudokeza mafumbo ya imani ili kuona yasiyoonekana.
Tanbihi
hariri- ↑ Bogomolets O. Radomysl Castle-Museum on the Royal Road Via Regia". — Kyiv, 2013 ISBN 978-617-7031-15-3
Marejeo
hariri- Beckwith, John, Early Christian and Byzantine Art, Penguin History of Art (now Yale), 2nd edn. 1979, ISBN 0-14-056033-5
Marejeo mengine
hariri- Evans, Helen C. (2004). Byzantium: faith and power (1261-1557). New York: The Metropolitan Museum of Art. ISBN 1-58839-113-2.
{{cite book}}
: External link in
(help)|title=
- Evans, Helen C. & Wixom, William D (1997). The glory of Byzantium: art and culture of the Middle Byzantine era, A.D. 843-1261. New York: The Metropolitan Museum of Art. ISBN 978-0-8109-6507-2.
{{cite book}}
: External link in
(help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)|title=
Viungo vya nje
hariri
Waorthodoksi
hariri- Orthodox Iconography by Elias Damianakis
- A Discourse in Iconography by St. John of Shanghai and San Francisco Ilihifadhiwa 11 Septemba 2011 kwenye Wayback Machine.
- The Iconic and Symbolic in Orthodox Iconography
- Icon & worship - Icons of Karakallou Monastery, Mt.Athos Ilihifadhiwa 18 Aprili 2014 kwenye Wayback Machine.
- Contemporary Byzantine icon studio, iconography school and orthodox resources Ilihifadhiwa 15 Mei 2011 kwenye Wayback Machine.
- Iconography Guide -free eLearning site Ilihifadhiwa 1 Agosti 2020 kwenye Wayback Machine.
- Orthodox iconography by Fr. Theodore Koufos Ilihifadhiwa 8 Mei 2011 kwenye Wayback Machine.
- On the difference of Western Religious Art and Orthodox Iconography Ilihifadhiwa 9 Oktoba 2015 kwenye Wayback Machine.
- Church of the Nativity - Explanation of Orthodox Christian Icons
- Concerning the Veneration of Icons
- Holy Icons: Theology in Color (Antiochian Orthodox Archdiocese)
- Icons by Sergei Fyodorov
- "Veneration of Images" article from The Catholic Encyclopedia
- Age of spirituality : late antique and early Christian art, third to seventh century from The Metropolitan Museum of Art
Picha
hariri- Icons of Mount Athos
- Greek Orthodox Archdiocese of America: Icons
- Gallery of icons, murals and mosaics (mostly Russian) from 11th to 20th century
- www.eikonografos.com A huge collection of Byzantine Icons
- Contemporary Orthodox Byzantine style murals. Large gallery. Ilihifadhiwa 15 Mei 2011 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Picha takatifu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |