Isidori wa Pelusio

Isidori wa Pelusio (kwa Kigiriki: Ἰσίδωρος ὁ Πηλουσιώτης; alifariki 450 hivi) alikuwa mmonaki padri wa Misri.

Isidori wa Pelusium.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Februari[1].

Maisha hariri

Mtoto pekee wa familia maarufu wa Aleksandria[2], akiwa ameshajipatia ujuzi mwingi, alitawa kwenye mlima karibu na mji wa Pelusium, kwa kufuata nyayo za Yohane Mbatizaji na Mababu wa jangwani.

Pia alijitosa kuhubiri kwa mfano wa Yohane Krisostomo akamtetea dhidi ya dhuluma kutoka kwa patriarki Theofilo wa Aleksandria, ndugu yake, na kwa malkia Eudosia.

Maandishi hariri

Anajulikana kwa barua 2,000 hivi alizowaandikia patriarki Sirili wa Aleksandria, kaisari Theodosius II na wengineo wengi.[3] Baadhi yake ni muhimu kwa ufafanuzi wa Biblia.[4]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Martyrologium Romanum
  2. Venerable Isidore of Pelusium (en).
  3. Pierre Evieux, Isidore de Peluse, 1995. A study of the man and his works, in French.
  4. C.H.Turner, The letters of Isidore of Pelusium, Journal of Theological Studies 6 (1905)

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.