Mchwa
Mchwa | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mchwa wafanya kazi na askari
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Familia 10:
|
Mchwa ni wadudu wadogo wa oda ya chini Isoptera katika oda Blattodea wanaoishi kwa makoloni makubwa katika vichuguu. Kuna aina ya mchwa ambao huishi ndani ya mbao au miti. Takriban spishi zote hula ubao.
Kila koloni lina malkia, mfalme, askari na wafanyakazi. Askari na wafanyakazi hawana mabawa lakini malkia na mfalme waliwahi kuwa na mabawa walipokuwa vijana. Mfalme anamtia malkia mbegu na huyu anazaa mayai mengi sana. Askari wanalinda kichuguu na wafanyakazi wanafanya kazi nyingine zote.
Mara kwa mara wafanyakazi wanawapatia majana kadhaa chakula fulani ili wawe wadudu wanaoweza kuzaa. Wadudu hawa wana mabawa na huitwa kumbikumbi.[1]
Utafiti wa hivi karibuni waonyesha mchwa, hasa mchwa wa Jangwa la Sahara, kuwa ndiye mnyama anayestahimili joto zaidi. Spishi hii ya mchwa inaweza kustahimili joto hadi nyuzi 55.1.[2]
Bidii na umoja
Mdudu huyu huishi kwa kushirikiana na kutangamana. Yeye halali kabla hajatafuta chakula cha kutosha na cha kuweka akiba.
Hivyo mchwa wametumika katika hadithi nyingi za kitoto ili kufunza maadili ya bidii na umoja. Kwa kawaida, mchwa hukaa wote pamoja katika koloni.
Mwandishi Aesop pia aliandika kuhusu bidii ya mchwa katika hadithi yake 'The Ant and the Grasshopper'.
Katika maandiko ya Biblia (kitabu cha Methali), waumini wameombwa waige mchwa katika utendakazi na umoja.
Katika kitabu kitakatifu cha Waislamu cha Kurani, Sulemani alisikia mchwa akiwaonya wengine warudi nyumbani wasije wakapondwapondwa.
Usumbufu wa mchwa
Hata hivyo, watu wengi huona mchwa kama wasumbufu, haswa anapoishi karibu na majengo ya watu. Mchwa hula mbao na kwa hiyo huharibu milango, samani na maboriti ya nyumba.
Wale wanaoishi ndani ya mbao na kula vifaa vya mbao nyumbani huleta pia tatizo la uchafu kutokana na kinyesi chao.[3] Kwa hiyo, watu wengi hutafuta dawa za kuua wadudu hawa au njia nyingine asili za kuwadhibiti kama vile utumizi wa udongo Diatomaceous au mafuta ya kitunguu saumu zinazoathiri wadudu[4].
Wanaofanya taaluma hiyo kwanza huangalia mchwa ni wa aina gani ili waweze kujua amejificha wapi maana wao hujifinya pahala kwingi.
Spishi kadhaa za Afrika
- Coptotermes amanii
- Cubitermes ugandensis
- Hodotermes mossambicus, Mchwa Mvunaji
- Macrotermes michaelseni, Mchwa Mkubwa wa Michaelsen
- Macrotermes natalensis
- Microtermes alluaudanus, Mchwa Mdogo wa Aluauda
- Pseudacanthoterms spiniger, Mchwa Miiba
- Odontotermes tanganicus, Mwcha-meno wa Tanga
- Trinervitermes trinervoides, Mchwa-pua Mvunaji
Picha
-
Kichuguu nchini Tanzania
-
Malkia
-
Mfanya kazi
-
Hodotermitidae (Hodotermes mossambicus)
-
Kalotermitidae (Cryptotermes brevis)
-
Mastotermitidae (Mastotermes darwiniensis)
-
Rhinotermitidae (Reticulitermes lucifugus)
-
Termitidae/Macrotermitinae (Odontotermes badius)
-
Termitidae/Nasutitermitinae (Nasutitermes corniger)
-
Termopsidae (Stolotermes ruficeps)
Tanbihi
- ↑ "Termite Larvae – What Does Baby Termite Look Like?". PestsGuide (kwa American English). 2018-11-24. Iliwekwa mnamo 2019-02-13.
- ↑ Nic Fleming. "The ant that is the hottest insect in the world". www.bbc.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-02-13.
- ↑ "Kuhusu kinyesi cha mchwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-07. Iliwekwa mnamo 2019-04-07. Ilihifadhiwa 7 Aprili 2019 kwenye Wayback Machine.
- ↑ Ambru (2018-11-24). "How to Get Rid of Termites: A Comprehensive Guide (2019)". PestsGuide (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-06-17.
Marejeo
- AntWeb from The California Academy of Sciences
- AntBase – a taxonomic database with literature sources
- AntWiki – Bringing Ants to the World
- Ant Species Fact Sheets from the National Pest Management Association on Argentine, Carpenter, Pharaoh, Odorous, and other ant species
- Ant Genera of the World – distribution maps
- The super-nettles. A dermatologist's guide to ants-in-the-plants
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mchwa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |